Zaburi 77:9-13
Zaburi 77:9-13 SRUV
Mungu amesahau fadhili zake? Amezuia kwa hasira rehema zake? Nikasema, Ndio udhaifu wangu huo; Lakini nitaikumbuka miaka ya mkono wa kulia wake Aliye Juu. Nitayakumbuka matendo ya BWANA; Naam, nitayakumbuka maajabu yako ya kale. Pia nitaitafakari kazi yako yote; Nitaziwaza habari za matendo yako. Ee Mungu, njia yako iko katika utakatifu; Ni Mungu yupi aliye mkuu kama Mungu wetu?