Zaburi 77:9-13
Zaburi 77:9-13 NEN
Je, Mungu amesahau kuwa na huruma? Je, katika hasira amezuia huruma yake?” Ndipo nikawaza, “Huu ndio udhaifu wangu: lakini nitakumbuka miaka ya mkono wa kuume wa Aliye Juu Sana.” Nitayakumbuka matendo ya BWANA; naam, nitaikumbuka miujiza yako ya zamani. Nitazitafakari kazi zako zote na kuyawaza matendo yako makuu. Ee Mungu, njia zako ni takatifu. Ni mungu yupi aliye mkuu kama Mungu wetu?