Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zab 77:9-13

Zab 77:9-13 SUV

Mungu amesahau fadhili zake? Amezuia kwa hasira rehema zake? Nikasema, Ndio udhaifu wangu huo; Lakini nitaikumbuka miaka ya mkono wa kuume wake Aliye juu. Nitayakumbuka matendo ya BWANA; Naam, nitayakumbuka maajabu yako ya kale. Pia nitaitafakari kazi yako yote; Nitaziwaza habari za matendo yako. Ee Mungu, njia yako i katika utakatifu; Ni nani aliye mungu mkuu kama Mungu?