Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zaburi 69:1-15

Zaburi 69:1-15 BHN

Uniokoe, ee Mungu; maji yamenifika shingoni. Ninazama ndani ya matope makuu, hamna hata mahali pa kuweka miguu. Nimetumbukia kwenye kilindi cha maji, nachukuliwa na mawimbi. Niko hoi kwa kupiga yowe, na koo langu limekauka. Macho yangu yamefifia, nikikungojea ewe Mungu wangu. Watu wengi kuliko nywele zangu ndio wanichukiao bure. Wana nguvu sana hao wanaotaka kuniua, hao wanaonishambulia kwa mambo ya uongo. Je, nirudishe kitu ambacho sikuiba? Ee Mungu, waujua upumbavu wangu; makosa yangu hayakufichika kwako. Wanaokutumainia wasiaibishwe kwa sababu yangu, ee Bwana Mwenyezi-Mungu wa majeshi; wanaokutafuta, wasione fedheha kwa sababu yangu ee Mungu wa Israeli. Kwa ajili yako nimefedheheshwa, aibu imefunika uso wangu. Nimekuwa mgeni kwa ndugu zangu, kaka na dada zangu hawanitambui. Upendo wangu kwa nyumba yako unanimaliza. Kashfa zote wanazokutolea wewe zimenipata mimi. Nilipojinyenyekesha kwa kufunga, watu walinilaumu. Nilipovaa vazi la gunia kuomboleza, wao walinidharau. Watu wananisengenya mabarabarani; walevi wanatunga nyimbo juu yangu. Lakini mimi nakuomba wewe, ee Mwenyezi-Mungu; nikubalie ombi langu wakati unaopenda, ee Mungu. Kwa wingi wa fadhili zako unijibu. Wewe ni mkombozi wa kuaminika. Kwa msaada wako amini uniokoe nisizame katika matope; uniokoe na hao wanaonichukia, unisalimishe kutoka vilindi vya maji. Usiniache nikumbwe na mkondo wa maji, au nizame kwenye kilindi au nimezwe na kifo.

Soma Zaburi 69