Zaburi 69:1-15
Zaburi 69:1-15 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Ee Mungu, uniokoe, Maana maji yamefika mpaka nafsini mwangu. Ninazama katika matope mengi, Pasipowezekana kusimama. Nimefika penye maji ya vilindi, Mkondo wa maji unanigharikisha. Nimechoka kwa kulia kwangu, Koo yangu imekauka. Macho yangu yamedhoofu Kwa kumngoja Mungu wangu. Wanaonichukia bure ni wengi Kuliko nywele za kichwa changu. Watakao kunikatilia mbali wamekuwa hodari, Adui zangu kwa sababu isiyo kweli. Hata mimi nalilipishwa kwa nguvu Vitu nisivyovichukua. Ee Mungu, unajua upumbavu wangu, Wala hukufichwa dhambi yangu. Wanaokungoja Wewe wasiaibishwe, Kwa ajili yangu, Bwana, MUNGU wa majeshi. Wanaokutafuta Wewe wasifedheheshwe, Kwa ajili yangu, Ee Mungu wa Israeli. Maana kwa ajili yako nimestahimili laumu, Fedheha imenifunika uso wangu. Nimekuwa mgeni kwa ndugu zangu, Na msikwao kwa wana wa mama yangu. Maana wivu wa nyumba yako umenila, Na laumu zao wanaokulaumu zimenipata. Nilipolia na kuiadhibu roho yangu kwa kufunga, Ikawa laumu juu yangu. Nilipofanya gunia kuwa nguo zangu, Nikawa mithali kwao. Waketio langoni hunisema, Na nyimbo za walevi hunidhihaki. Nami maombi yangu nakuomba Wewe, BWANA, Wakati ukupendezao; Ee Mungu, Kwa wingi wa fadhili zako unijibu, Katika kweli ya wokovu wako. Uniponye kwa kunitoa matopeni, Wala usiniache nikazama. Na niponywe nao wanaonichukia, Na katika vilindi vya maji. Mkondo usinigharikishe, wala vilindi visinimeze, Wala shimo lisifumbe kinywa chake juu yangu.
Zaburi 69:1-15 Biblia Habari Njema (BHN)
Uniokoe, ee Mungu; maji yamenifika shingoni. Ninazama ndani ya matope makuu, hamna hata mahali pa kuweka miguu. Nimetumbukia kwenye kilindi cha maji, nachukuliwa na mawimbi. Niko hoi kwa kupiga yowe, na koo langu limekauka. Macho yangu yamefifia, nikikungojea ewe Mungu wangu. Watu wengi kuliko nywele zangu ndio wanichukiao bure. Wana nguvu sana hao wanaotaka kuniua, hao wanaonishambulia kwa mambo ya uongo. Je, nirudishe kitu ambacho sikuiba? Ee Mungu, waujua upumbavu wangu; makosa yangu hayakufichika kwako. Wanaokutumainia wasiaibishwe kwa sababu yangu, ee Bwana Mwenyezi-Mungu wa majeshi; wanaokutafuta, wasione fedheha kwa sababu yangu ee Mungu wa Israeli. Kwa ajili yako nimefedheheshwa, aibu imefunika uso wangu. Nimekuwa mgeni kwa ndugu zangu, kaka na dada zangu hawanitambui. Upendo wangu kwa nyumba yako unanimaliza. Kashfa zote wanazokutolea wewe zimenipata mimi. Nilipojinyenyekesha kwa kufunga, watu walinilaumu. Nilipovaa vazi la gunia kuomboleza, wao walinidharau. Watu wananisengenya mabarabarani; walevi wanatunga nyimbo juu yangu. Lakini mimi nakuomba wewe, ee Mwenyezi-Mungu; nikubalie ombi langu wakati unaopenda, ee Mungu. Kwa wingi wa fadhili zako unijibu. Wewe ni mkombozi wa kuaminika. Kwa msaada wako amini uniokoe nisizame katika matope; uniokoe na hao wanaonichukia, unisalimishe kutoka vilindi vya maji. Usiniache nikumbwe na mkondo wa maji, au nizame kwenye kilindi au nimezwe na kifo.
Zaburi 69:1-15 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Ee Mungu, uniokoe, Maana maji yamefika mpaka nafsini mwangu. Ninazama katika matope mengi, Pasipowezekana kusimama. Nimefika penye maji ya vilindi, Mkondo wa maji unanigharikisha. Nimechoka kwa kulia kwangu, Koo yangu imekauka. Macho yangu yamedhoofika Kwa kumngoja Mungu wangu. Wanaonichukia bure ni wengi Kuliko nywele za kichwa changu. Watakao kunikatilia mbali ni wengi, Adui zangu kwa sababu isiyo kweli. Hata mimi nililipishwa kwa nguvu Vitu nisivyovichukua. Ee Mungu, unajua upumbavu wangu, Wala hukufichwa dhambi yangu. Wanaokungoja Wewe wasiaibishwe, Kwa ajili yangu, Bwana, MUNGU wa majeshi. Wanaokutafuta Wewe wasifedheheshwe, Kwa ajili yangu, Ee Mungu wa Israeli. Maana kwa ajili yako nimestahimili laumu, Fedheha imenifunika uso wangu. Nimekuwa mgeni kwa ndugu zangu, Na asiyetambuliwa na wana wa mama yangu. Maana mvuto wa nyumba yako umenila, Na laumu zao wanaokulaumu zimenipata. Nilipolia na kuiadhibu roho yangu kwa kufunga, Nikalaumiwa kwa hayo. Nilipofanya gunia kuwa nguo zangu, Nikawa kifani cha dharau kwao. Waketio langoni hunisema, Na nyimbo za walevi hunidhihaki. Nami maombi yangu nakuomba Wewe, BWANA, Wakati ukupendezao; Ee Mungu, Kwa wingi wa fadhili zako unijibu, Katika kweli ya wokovu wako. Uniponye kwa kunitoa matopeni, Wala usiniache nikazama. Na niponywe kutoka kwa wanaonichukia, Na kutoka katika vilindi vya maji. Mkondo usinigharikishe, wala vilindi visinimeze, Wala Shimo lisifumbe kinywa chake juu yangu.
Zaburi 69:1-15 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Ee Mungu, uniokoe, Maana maji yamefika mpaka nafsini mwangu. Ninazama katika matope mengi, Pasipowezekana kusimama. Nimefika penye maji ya vilindi, Mkondo wa maji unanigharikisha. Nimechoka kwa kulia kwangu, Koo yangu imekauka. Macho yangu yamedhoofu Kwa kumngoja Mungu wangu. Wanaonichukia bure ni wengi Kuliko nywele za kichwa changu. Watakao kunikatilia mbali wamekuwa hodari, Adui zangu kwa sababu isiyo kweli. Hata mimi nalilipishwa kwa nguvu Vitu nisivyovichukua. Ee Mungu, unajua upumbavu wangu, Wala hukufichwa dhambi yangu. Wanaokungoja Wewe wasiaibishwe, Kwa ajili yangu, Bwana, MUNGU wa majeshi. Wanaokutafuta Wewe wasifedheheshwe, Kwa ajili yangu, Ee Mungu wa Israeli. Maana kwa ajili yako nimestahimili laumu, Fedheha imenifunika uso wangu. Nimekuwa mgeni kwa ndugu zangu, Na msikwao kwa wana wa mama yangu. Maana wivu wa nyumba yako umenila, Na laumu zao wanaokulaumu zimenipata. Nilipolia na kuiadhibu roho yangu kwa kufunga, Ikawa laumu juu yangu. Nilipofanya gunia kuwa nguo zangu, Nikawa mithali kwao. Waketio langoni hunisema, Na nyimbo za walevi hunidhihaki. Nami maombi yangu nakuomba Wewe, BWANA, Wakati ukupendezao; Ee Mungu, Kwa wingi wa fadhili zako unijibu, Katika kweli ya wokovu wako. Uniponye kwa kunitoa matopeni, Wala usiniache nikazama. Na niponywe nao wanaonichukia, Na katika vilindi vya maji. Mkondo usinigharikishe, wala vilindi visinimeze, Wala shimo lisifumbe kinywa chake juu yangu.
Zaburi 69:1-15 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Ee Mungu, niokoe, kwa maana maji yamenifika shingoni. Ninazama kwenye vilindi vya matope, pasipo mahali pa kukanyaga, Nimefika kwenye maji makuu, mafuriko yamenigharikisha. Nimechoka kwa kuomba msaada, koo langu limekauka. Macho yangu yanafifia, nikimtafuta Mungu wangu. Wale wanaonichukia bila sababu ni wengi kuliko nywele za kichwa changu; wengi ni adui kwangu bila sababu, wale wanaotafuta kuniangamiza. Ninalazimishwa kurudisha kitu ambacho sikuiba. Ee Mungu, wewe unajua upumbavu wangu, wala hatia yangu haikufichika kwako. Ee Bwana, ewe BWANA Mwenye Nguvu Zote, wakutumainio wasiaibishwe kwa ajili yangu; wakutafutao wasifedheheshwe kwa ajili yangu, Ee Mungu wa Israeli. Kwa maana nimestahimili dharau kwa ajili yako, aibu imefunika uso wangu. Nimekuwa mgeni kwa ndugu zangu, mgeni kwa wana wa mama yangu mwenyewe. Kwa kuwa wivu wa nyumba yako unanila, matukano ya wale wanaokutukana yameniangukia. Ninapolia na kufunga, lazima nivumilie matusi. Ninapovaa nguo ya gunia, watu hunidharau. Wale wanaoketi mlangoni wananisimanga, nimekuwa wimbo wa walevi. Lakini Ee BWANA, ninakuomba, kwa wakati ukupendezao; katika upendo wako mkuu, Ee Mungu, unijibu kwa wokovu wako wa hakika. Uniokoe katika matope, usiniache nizame; niokoe na hao wanichukiao, kutoka kwenye vilindi vya maji. Usiache mafuriko yanigharikishe au vilindi vinimeze, au shimo lifumbe kinywa chake juu yangu.