Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zab 69

69
Sala ya Ukombozi katika Mateso
Kwa mwimbishaji: kwa mtindo wa Yungiyungi. Ya Daudi.
1Ee Mungu, uniokoe,
Maana maji yamefika mpaka nafsini mwangu.
2Ninazama katika matope mengi,
Pasipowezekana kusimama.
Nimefika penye maji ya vilindi,
Mkondo wa maji unanigharikisha.
3Nimechoka kwa kulia kwangu,
Koo yangu imekauka.
Macho yangu yamedhoofu
Kwa kumngoja Mungu wangu.
4 # Zab 35:19; Yn 15:25 Wanaonichukia bure ni wengi
Kuliko nywele za kichwa changu.
Watakao kunikatilia mbali wamekuwa hodari,
Adui zangu kwa sababu isiyo kweli.
Hata mimi nalilipishwa kwa nguvu
Vitu nisivyovichukua.
5Ee Mungu, unajua upumbavu wangu,
Wala hukufichwa dhambi yangu.
6Wanaokungoja Wewe wasiaibishwe,
Kwa ajili yangu, Bwana, MUNGU wa majeshi.
Wanaokutafuta Wewe wasifedheheshwe,
Kwa ajili yangu, Ee Mungu wa Israeli.
7Maana kwa ajili yako nimestahimili laumu,
Fedheha imenifunika uso wangu.
8 # Isa 53:3; Yn 1:11 Nimekuwa mgeni kwa ndugu zangu,
Na msikwao kwa wana wa mama yangu.
9 # 1 Fal 19:10; Zab 119:139; Yn 2:17; Rum 15:3 Maana wivu wa nyumba yako umenila,
Na laumu zao wanaokulaumu zimenipata.
10Nilipolia na kuiadhibu roho yangu kwa kufunga,
Ikawa laumu juu yangu.
11 # 1 Fal 9:7; Yer 24:9; Zab 44:13,14 Nilipofanya gunia kuwa nguo zangu,
Nikawa mithali kwao.
12 # Ayu 17:6; Omb 3:14 Waketio langoni hunisema,
Na nyimbo za walevi hunidhihaki.
13 # Isa 49:8; 2 Kor 6:2 Nami maombi yangu nakuomba Wewe, BWANA,
Wakati ukupendezao; Ee Mungu,
Kwa wingi wa fadhili zako unijibu,
Katika kweli ya wokovu wako.
14Uniponye kwa kunitoa matopeni,
Wala usiniache nikazama.
Na niponywe nao wanaonichukia,
Na katika vilindi vya maji.
15Mkondo usinigharikishe, wala vilindi visinimeze,
Wala shimo lisifumbe kinywa chake juu yangu.
16Ee BWANA, unijibu, maana fadhili zako ni njema,
Kwa kadiri ya rehema zako unielekee.
17Wala usinifiche uso wako, mimi mtumishi wako,
Maana mimi nimo taabuni, unijibu upesi.
18Uikaribie nafsi yangu, uikomboe,
Kwa sababu ya adui zangu unifidie.
19 # Zab 22:6; Isa 53:3; Ebr 12:2 Wewe umejua kulaumiwa kwangu,
Na kuaibika na kufedheheka kwangu,
Mbele zako Wewe wako watesi wangu wote.
20Laumu imenivunja moyo,
Nami ninaugua sana.
Nikangoja aje wa kunihurumia, wala hakuna;
Na wa kunifariji, wala sikumwona mtu.
21 # Mt 27:34; 27:48; Mk 15:36; Lk 23:36; Yn 19:28-29 Wakanipa uchungu kuwa chakula changu;
Nami nilipokuwa na kiu wakaninywesha siki.
22 # Rum 11:9-10; 2 Kor 3:14 Meza yao mbele yao na iwe mtego;
Naam, wakiwa salama na iwe tanzi.
23Macho yao yatiwe giza wasione,
Na viuno vyao uvitetemeshe daima.
24Uimwage ghadhabu yako juu yao,
Na ukali wa hasira yako uwapate.
25 # Mdo 1:20 Matuo yao na yawe ukiwa,
Pasiwe na mtu wa kukaa hemani mwao.
26 # Isa 53:4 Maana wanamwudhi mtu uliyempiga Wewe,
Wanasimulia maumivu ya hao uliowatia jeraha.
27 # Rum 9:31 Uwaongezee uovu juu ya uovu,
Wala wasiingie katika haki yako.
28 # Kut 32:32; Eze 13:9; Lk 10:20; Flp 4:3; Ebr 12:23; Ufu 3:5; 13:8; 17:8 Na wafutwe katika chuo cha uhai,
Wala pamoja na wenye haki wasiandikwe.
29Nami niliye maskini na mtu wa huzuni,
Mungu, wokovu wako utaniinua.
30Nitalisifu jina la Mungu kwa wimbo,
Nami nitamtukuza kwa shukrani.
31Nayo yatampendeza BWANA kuliko ng’ombe,
Au ndama mwenye pembe na kwato.
32Walioonewa watakapoona watafurahi;
Enyi mmtafutao Mungu, mioyo yenu ihuishwe.
33Kwa kuwa BWANA huwasikia wahitaji,
Wala hawadharau wafungwa wake.
34Mbingu na nchi zimsifu,
Bahari na vyote viendavyo ndani yake.
35 # Zab 51:18; 102:13,16; Isa 14:32; 44:26 Maana Mungu ataiokoa Sayuni, na kuijenga miji ya Yuda,
Na watu watakaa ndani yake na kuimiliki.
36Wazao wa watumishi wake watairithi,
Nao walipendao jina lake watakaa humo.

Iliyochaguliwa sasa

Zab 69: SUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha