Zaburi 61:1-4
Zaburi 61:1-4 BHN
Ee Mungu, usikie kilio changu, usikilize sala yangu. Ninakulilia kutoka miisho ya dunia, nikiwa nimevunjika moyo. Uniongoze juu kwenye mwamba mkubwa maana wewe ndiwe kimbilio langu, kinga yangu imara dhidi ya adui. Naomba nikae nyumbani mwako milele nipate usalama chini ya mabawa yako.