Zaburi 61:1-4
Zaburi 61:1-4 Biblia Habari Njema (BHN)
Ee Mungu, usikie kilio changu, usikilize sala yangu. Ninakulilia kutoka miisho ya dunia, nikiwa nimevunjika moyo. Uniongoze juu kwenye mwamba mkubwa maana wewe ndiwe kimbilio langu, kinga yangu imara dhidi ya adui. Naomba nikae nyumbani mwako milele nipate usalama chini ya mabawa yako.
Zaburi 61:1-4 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Ee Mungu, ukisikie kilio changu, Uyasikilize maombi yangu. Toka mwisho wa nchi nitakulilia nikizimia moyo, Uniongoze juu ya mwamba nisioweza kuupanda. Kwa maana ulikuwa kimbilio langu, Ngome yenye nguvu adui asinipate. Nitakaa katika hema yako milele, Nitaikimbilia sitara ya mbawa zako
Zaburi 61:1-4 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Ee Mungu, sikia kilio changu, usikilize maombi yangu. Kutoka miisho ya dunia ninakuita, ninaita huku moyo wangu unadhoofika; uniongoze kwenye mwamba ule ulio juu kuliko mimi. Kwa kuwa umekuwa kimbilio langu, ngome imara dhidi ya adui. Natamani kukaa hemani mwako milele, na kukimbilia chini ya uvuli wa mbawa zako.

Zaburi 61:1-4 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Ee Mungu, ukisikie kilio changu, Uyasikilize maombi yangu. Toka mwisho wa nchi nitakulilia ninapozimia moyo, Uniongoze juu ya mwamba nisioweza kuupanda. Kwa maana ulikuwa kimbilio langu, Ngome yenye nguvu adui asinipate. Nitakaa katika hema yako milele, Na kupata kimbilio chini ya mbawa zako.