Zaburi 61:1-4
Zaburi 61:1-4 SRUV
Ee Mungu, ukisikie kilio changu, Uyasikilize maombi yangu. Toka mwisho wa nchi nitakulilia ninapozimia moyo, Uniongoze juu ya mwamba nisioweza kuupanda. Kwa maana ulikuwa kimbilio langu, Ngome yenye nguvu adui asinipate. Nitakaa katika hema yako milele, Na kupata kimbilio chini ya mbawa zako.