Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zaburi 61:1-4

Zaburi 61:1-4 NEN

Ee Mungu, sikia kilio changu, usikilize maombi yangu. Kutoka miisho ya dunia ninakuita, ninaita huku moyo wangu unadhoofika; uniongoze kwenye mwamba ule ulio juu kuliko mimi. Kwa kuwa umekuwa kimbilio langu, ngome imara dhidi ya adui. Natamani kukaa hemani mwako milele, na kukimbilia chini ya uvuli wa mbawa zako.