Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zaburi 140:1-13

Zaburi 140:1-13 BHN

Ee Mwenyezi-Mungu, uniokoe na watu wabaya, unikinge na watu wakatili. Watu hao huwaza mabaya daima, huzusha magomvi kila mara. Ndimi zao hatari kama za nyoka; midomoni mwao mna maneno ya sumu kama ya joka. Ee Mwenyezi-Mungu, unilinde na makucha ya wabaya; unikinge na watu wakatili ambao wamepanga kuniangusha. Wenye kiburi wamenitegea mitego, wametandaza kamba kama wavu, wameficha mitego njiani wanikamate. Namwambia Mwenyezi-Mungu, “Wewe ndiwe Mungu wangu.” Usikilize, ee Mwenyezi-Mungu, sauti ya ombi langu. Ee Mwenyezi-Mungu, Bwana wangu, mkombozi wangu mkuu, umenikinga salama wakati wa vita. Ee Mwenyezi-Mungu, usiwape waovu wanayotaka; wala mipango yao mibaya usiifanikishe. Hao wanaonizingira wanainua vichwa; uovu wa maneno yao uwapate wao wenyewe! Makaa ya moto yawaangukie; watumbukizwe mashimoni, wasiinuke tena. Wanaowasengenya wengine wasifanikiwe katika nchi; uovu uwapate wakatili na kuwaangamiza mara! Najua Mwenyezi-Mungu hutetea kisa cha wanaoteswa, na kuwapatia haki maskini. Hakika waadilifu watalisifu jina lako; wanyofu watakaa kwako.

Soma Zaburi 140