Zaburi 140:1-13
Zaburi 140:1-13 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Ee BWANA, uniokoe kutoka kwa watu waovu. Unihifadhi kutoka kwa watu wajeuri. Waliowaza mabaya mioyoni mwao, Kila siku huchochea vita. Wamenoa ndimi zao na kuwa kama za nyoka, Na katika midomo yao mna sumu ya fira. Ee BWANA, unilinde Kutoka kwa mikono ya mtu asiye haki; Unihifadhi na watu wajeuri; Waliopanga kuniangusha. Wenye kiburi wamenifichia mtego na kamba; Wametandika wavu kando ya njia; Wameniwekea matanzi. Nimemwambia BWANA, Ndiwe Mungu wangu; Ee BWANA, uisikie sauti ya dua zangu. Ee MUNGU Bwana, nguvu za wokovu wangu, Umenifunika kichwa changu siku ya vita. Ee BWANA, usimpe asiye haki tamaa zake, Usiifanikishe hila yake, wasije wakajiinua. Nao wainuapo vichwa watu wanaonizunguka, Madhara ya midomo yao yawafunike. Makaa ya moto yawaangukie, watupwe motoni, Na katika mashimo, wasipate kusimama tena. Msingiziaji hatawekwa imara katika nchi, Mtu wa jeuri, uovu humwinda kumwangamiza. Najua ya kuwa BWANA atamfanyia mnyonge hukumu, Na wahitaji haki yao. Hakika wenye haki watalishukuru jina lako, Wenye adili watakaa mahali ulipo Wewe.
Zaburi 140:1-13 Biblia Habari Njema (BHN)
Ee Mwenyezi-Mungu, uniokoe na watu wabaya, unikinge na watu wakatili. Watu hao huwaza mabaya daima, huzusha magomvi kila mara. Ndimi zao hatari kama za nyoka; midomoni mwao mna maneno ya sumu kama ya joka. Ee Mwenyezi-Mungu, unilinde na makucha ya wabaya; unikinge na watu wakatili ambao wamepanga kuniangusha. Wenye kiburi wamenitegea mitego, wametandaza kamba kama wavu, wameficha mitego njiani wanikamate. Namwambia Mwenyezi-Mungu, “Wewe ndiwe Mungu wangu.” Usikilize, ee Mwenyezi-Mungu, sauti ya ombi langu. Ee Mwenyezi-Mungu, Bwana wangu, mkombozi wangu mkuu, umenikinga salama wakati wa vita. Ee Mwenyezi-Mungu, usiwape waovu wanayotaka; wala mipango yao mibaya usiifanikishe. Hao wanaonizingira wanainua vichwa; uovu wa maneno yao uwapate wao wenyewe! Makaa ya moto yawaangukie; watumbukizwe mashimoni, wasiinuke tena. Wanaowasengenya wengine wasifanikiwe katika nchi; uovu uwapate wakatili na kuwaangamiza mara! Najua Mwenyezi-Mungu hutetea kisa cha wanaoteswa, na kuwapatia haki maskini. Hakika waadilifu watalisifu jina lako; wanyofu watakaa kwako.
Zaburi 140:1-13 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Ee BWANA, uniokoe kutoka kwa watu waovu. Unihifadhi kutoka kwa watu wajeuri. Waliowaza mabaya mioyoni mwao, Kila siku huchochea vita. Wamenoa ndimi zao na kuwa kama za nyoka, Na katika midomo yao mna sumu ya fira. Ee BWANA, unilinde Kutoka kwa mikono ya mtu asiye haki; Unihifadhi na watu wajeuri; Waliopanga kuniangusha. Wenye kiburi wamenifichia mtego na kamba; Wametandika wavu kando ya njia; Wameniwekea matanzi. Nimemwambia BWANA, Ndiwe Mungu wangu; Ee BWANA, uisikie sauti ya dua zangu. Ee MUNGU Bwana, nguvu za wokovu wangu, Umenifunika kichwa changu siku ya vita. Ee BWANA, usimpe asiye haki tamaa zake, Usiifanikishe hila yake, wasije wakajiinua. Nao wainuapo vichwa watu wanaonizunguka, Madhara ya midomo yao yawafunike. Makaa ya moto yawaangukie, watupwe motoni, Na katika mashimo, wasipate kusimama tena. Msingiziaji hatawekwa imara katika nchi, Mtu wa jeuri, uovu humwinda kumwangamiza. Najua ya kuwa BWANA atamfanyia mnyonge hukumu, Na wahitaji haki yao. Hakika wenye haki watalishukuru jina lako, Wenye adili watakaa mahali ulipo Wewe.
Zaburi 140:1-13 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Ee BWANA, uniokoe na mtu mbaya, Unihifadhi na mtu wa jeuri. Waliowaza mabaya mioyoni mwao, Kila siku huondokesha vita. Wamenoa ndimi zao kama nyoka, Sumu ya fira i chini ya midomo yao. Ee BWANA, unilinde na mikono ya mtu asiye haki; Unihifadhi na mtu wa jeuri; Waliowaza kuzipotosha hatua zangu. Wenye kiburi wamenifichia mtego na kamba; Wametandika wavu kando ya njia; Wameniwekea matanzi. Nimemwambia BWANA, Ndiwe Mungu wangu; Ee BWANA, uisikie sauti ya dua zangu. Ee MUNGU Bwana, nguvu za wokovu wangu, Umenifunika kichwa changu siku ya vita. Ee BWANA, usimpe asiye haki tamaa zake, Usiifanikishe hila yake, wasije wakajiinua. Nao wainuapo vichwa watu wanaonizunguka, Madhara ya midomo yao yawafunike. Makaa ya moto yawaangukie, watupwe motoni, Na katika mashimo, wasipate kusimama tena. Msingiziaji hatawekwa imara katika nchi, Mtu wa jeuri, uovu humwinda kumwangamiza. Najua ya kuwa BWANA atamfanyia mnyonge hukumu, Na wahitaji haki yao. Hakika wenye haki watalishukuru jina lako, Wenye adili watakaa mahali ulipo Wewe.
Zaburi 140:1-13 Neno: Maandiko Matakatifu 2024 (NENO)
Ee Mwenyezi Mungu, niokoe, kutoka kwa watu waovu; nilinde na watu wenye jeuri, ambao hupanga mipango mibaya mioyoni mwao, na kuchochea vita siku zote. Wao hufanya ndimi zao kali kama za nyoka, sumu ya nyoka iko midomoni mwao. Ee Mwenyezi Mungu, niepushe na mikono ya waovu; nilinde na watu wenye jeuri wanaopanga kunikwaza miguu yangu. Wenye kiburi wameficha mtego wa kuninasa, wametandaza kamba za wavu wao, wametega mitego kwenye njia yangu. Ee Mwenyezi Mungu, ninakuambia, “Wewe ni Mungu wangu.” Ee Mwenyezi Mungu, usikie kilio changu na kunihurumia. Ee Bwana Mungu Mwenyezi, Mwokozi wangu mwenye nguvu, unikingaye kichwa changu siku ya vita: Ee Mwenyezi Mungu, usiwape waovu matakwa yao, usiache mipango yao ikafanikiwa, wasije wakajisifu. Vichwa vya wanaonizunguka vifunikwe na shida zilizosababishwa na midomo yao. Makaa ya mawe ya moto na yawaangukie! Na watupwe motoni, katika mashimo ya matope, wasiinuke tena kamwe. Wasingiziaji wasifanikiwe katika nchi; maafa na yawawinde watu wenye jeuri. Najua kwamba Mwenyezi Mungu huwapatia maskini haki, na kuitegemeza njia ya mhitaji. Hakika wenye haki watalisifu jina lako, na waadilifu wataishi mbele zako.