Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Methali 30:7-17

Methali 30:7-17 BHN

Mambo haya mawili nakuomba ee Mungu, wala usinikatalie kabla sijafa: Uniondolee uongo na udanganyifu; usinipe umaskini wala utajiri; unipatie chakula ninachohitaji, nisije nikashiba nikakukana; nikasema, “Mwenyezi-Mungu ni nani?” Au nisije nikawa maskini nikaiba, na kulikufuru jina lako ee Mungu wangu. Usimchongee mtumwa kwa bwana wake, asije akakulaani, ukaonekana una hatia. Kuna watu ambao huwalaani baba zao, wala hawana shukrani kwa mama zao. Kuna watu ambao hujiona kuwa wema, kumbe bado hawajatakaswa uchafu wao. Kuna na wengine – kiburi ajabu! Hudharau kila kitu wanachokiona. Kuna watu ambao meno yao ni kama upanga, na magego yao ni kama visu. Wako tayari kuwatafuna maskini wa nchi, na wanyonge walio miongoni mwa watu! Mruba anao binti wawili wasemao, “Nipe, nipe!” Kuna vitu vitatu ambavyo kamwe havishibi, naam, vitu vinne visivyosema, “Imetosha!” Kuzimu, tumbo la mwanamke lisilozaa, ardhi isiyoshiba maji, na moto usiosema, “Imetosha!” Kama mtu akimdhihaki baba yake, na kudharau utii kwa mama yake, kunguru wa bondeni watamdonoa macho, na kuliwa na tai.

Soma Methali 30