Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Mithali 30:7-17

Mithali 30:7-17 SRUV

Mambo haya mawili nimekuomba; Usininyime [matatu] kabla sijafa. Uniondolee ubatili na uongo; Usinipe umaskini wala utajiri; Unilishe chakula kilicho kadiri yangu. Nisije nikashiba nikakukana, Nikasema, BWANA ni nani? Wala nisiwe maskini sana nikaiba, Na kulitaja bure jina la Mungu wangu. Usimchongee mtumwa kwa bwana wake; Asije akakulaani, ukaonekana una hatia. Kuna kizazi cha watu wamlaanio baba yao; Wala hawambariki mama yao. Kuna kizazi cha watu walio safi machoni pao wenyewe; Ambao hawakuoshwa uchafu wao. Kuna kizazi cha watu ambao macho yao yameinuka kama nini! Na kope zao zimeinuka sana. Kuna kizazi cha watu ambao meno yao ni panga; Na vigego vyao ni kama visu. Ili kuwala maskini waondolewe katika nchi, Na wahitaji katika wanadamu. Mruba anao binti wawili, Waliao, Nipe! Nipe! Kuna vitu vitatu visivyoshiba kamwe, Naam, vinne visivyosema, Basi! Kuzimu; na tumbo lisilozaa; Nchi isiyoshiba maji; na moto usiosema, Basi! Jicho la mtu amdhihakiye babaye, Na kudharau kumtii mamaye; Kunguru wa bondeni wataling'oa, Na vifaranga vya tai watalila.

Soma Mithali 30