Methali 30:7-17
Methali 30:7-17 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Mambo haya mawili nimekuomba; Usininyime [matatu] kabla sijafa. Uniondolee ubatili na uongo; Usinipe umaskini wala utajiri; Unilishe chakula kilicho kadiri yangu. Nisije nikashiba nikakukana, Nikasema, BWANA ni nani? Wala nisiwe maskini sana nikaiba, Na kulitaja bure jina la Mungu wangu. Usimchongee mtumwa kwa bwana wake; Asije akakulaani, ukaonekana una hatia. Kuna kizazi cha watu wamlaanio baba yao; Wala hawambariki mama yao. Kuna kizazi cha watu walio safi machoni pao wenyewe; Ambao hawakuoshwa uchafu wao. Kuna kizazi cha watu ambao macho yao yameinuka kama nini! Na kope zao zimeinuka sana. Kuna kizazi cha watu ambao meno yao ni panga; Na vigego vyao ni kama visu. Ili kuwala maskini waondolewe katika nchi, Na wahitaji katika wanadamu. Mruba anao binti wawili, Waliao, Nipe! Nipe! Kuna vitu vitatu visivyoshiba kamwe, Naam, vinne visivyosema, Basi! Kuzimu; na tumbo lisilozaa; Nchi isiyoshiba maji; na moto usiosema, Basi! Jicho la mtu amdhihakiye babaye, Na kudharau kumtii mamaye; Kunguru wa bondeni wataling'oa, Na vifaranga vya tai watalila.
Methali 30:7-17 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Mambo haya mawili nimekuomba; Usininyime [matatu] kabla sijafa. Uniondolee ubatili na uongo; Usinipe umaskini wala utajiri; Unilishe chakula kilicho kadiri yangu. Nisije nikashiba nikakukana, Nikasema, BWANA ni nani? Wala nisiwe maskini sana nikaiba, Na kulitaja bure jina la Mungu wangu. Usimchongee mtumwa kwa bwana wake; Asije akakulaani, ukaonekana una hatia. Kuna kizazi cha watu wamlaanio baba yao; Wala hawambariki mama yao. Kuna kizazi cha watu walio safi machoni pao wenyewe; Ambao hawakuoshwa uchafu wao. Kuna kizazi cha watu ambao macho yao yameinuka kama nini! Na kope zao zimeinuka sana. Kuna kizazi cha watu ambao meno yao ni panga; Na vigego vyao ni kama visu. Ili kuwala maskini waondolewe katika nchi, Na wahitaji katika wanadamu. Mruba anao binti wawili, Waliao, Nipe! Nipe! Kuna vitu vitatu visivyoshiba kamwe, Naam, vinne visivyosema, Basi! Kuzimu; na tumbo lisilozaa; Nchi isiyoshiba maji; na moto usiosema, Basi! Jicho la mtu amdhihakiye babaye, Na kudharau kumtii mamaye; Kunguru wa bondeni wataling’oa, Na vifaranga vya tai watalila.
Methali 30:7-17 Biblia Habari Njema (BHN)
Mambo haya mawili nakuomba ee Mungu, wala usinikatalie kabla sijafa: Uniondolee uongo na udanganyifu; usinipe umaskini wala utajiri; unipatie chakula ninachohitaji, nisije nikashiba nikakukana; nikasema, “Mwenyezi-Mungu ni nani?” Au nisije nikawa maskini nikaiba, na kulikufuru jina lako ee Mungu wangu. Usimchongee mtumwa kwa bwana wake, asije akakulaani, ukaonekana una hatia. Kuna watu ambao huwalaani baba zao, wala hawana shukrani kwa mama zao. Kuna watu ambao hujiona kuwa wema, kumbe bado hawajatakaswa uchafu wao. Kuna na wengine – kiburi ajabu! Hudharau kila kitu wanachokiona. Kuna watu ambao meno yao ni kama upanga, na magego yao ni kama visu. Wako tayari kuwatafuna maskini wa nchi, na wanyonge walio miongoni mwa watu! Mruba anao binti wawili wasemao, “Nipe, nipe!” Kuna vitu vitatu ambavyo kamwe havishibi, naam, vitu vinne visivyosema, “Imetosha!” Kuzimu, tumbo la mwanamke lisilozaa, ardhi isiyoshiba maji, na moto usiosema, “Imetosha!” Kama mtu akimdhihaki baba yake, na kudharau utii kwa mama yake, kunguru wa bondeni watamdonoa macho, na kuliwa na tai.
Methali 30:7-17 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
“Ninakuomba vitu viwili, Ee BWANA; usininyime kabla sijafa: Uutenge mbali nami udanganyifu na uongo; usinipe umaskini wala utajiri, bali unipe chakula cha kunitosha kila siku. Nisije nikawa na vingi vya kuzidi nikakukana na kusema, ‘BWANA ni nani?’ Au nisije nikawa maskini nikaiba, nami nikaliaibisha jina la Mungu wangu. “Usimchongee mtumishi kwa bwana wake, asije akakulaani, ukapatilizwa kwalo. “Wako watu wale ambao huwalaani baba zao na wala hawawabariki mama zao; wale ambao ni safi machoni pao wenyewe kumbe hawakuoshwa uchafu wao; wale ambao daima macho yao ni ya kiburi, ambao kutazama kwao ni kwa dharau; wale ambao meno yao ni panga na ambao mataya yao yamewekwa visu kuwaangamiza maskini katika nchi, na wahitaji kutoka miongoni mwa wanadamu. “Mruba anao binti wawili waliao, ‘Nipe! Nipe!’ “Kuna vitu vitatu visivyotosheka kamwe, naam, viko vinne visivyosema, ‘Yatosha!’: Ni kaburi, tumbo lisilozaa, nchi isiyoshiba maji kamwe, na moto, usiosema kamwe, ‘Yatosha!’ “Jicho lile limdhihakilo baba, lile linalodharau kumtii mama, litangʼolewa na kunguru wa bondeni, litaliwa na tai.