Zaburi 72:1-4
Zaburi 72:1-4 SRUV
Ee Mungu, mpe mfalme hukumu zako, Na mwana wa mfalme haki yako. Atawaamua watu wako kwa haki, Na watu wako walioonewa kwa hukumu. Milimana iwaletee watu amani, Na pamoja na vilima, ilete haki. Na atawatetea watu walioonewa, Awaokoe wahitaji, na kumwaangamiza mdhalimu.