Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Mithali 12:11-23

Mithali 12:11-23 SRUV

Alimaye shamba lake atakuwa na chakula tele; Bali afuataye mambo ya upuzi hana ufahamu. Asiye haki hutamani nyavu za wabaya; Bali shina lao wenye haki huleta matunda. Katika kosa la midomo kuna mtego kwa mbaya; Bali mwenye haki atatoka katika taabu. Mtu atashiba mema kwa matunda ya kinywa chake; Na atarudishiwa matendo ya mikono yake. Njia ya mpumbavu imenyoka machoni pake mwenyewe; Bali yeye aliye na hekima husikiliza shauri. Ghadhabu ya mpumbavu hujulikana mara; Bali mtu mwerevu husitiri aibu. Atamkaye maneno ya kweli hufunua haki; Bali shahidi wa uongo hutamka hila. Kuna anenaye bila kufikiri, kama kuchoma kwa upanga; Bali ulimi wa mwenye haki ni afya. Mdomo wa kweli utathibitishwa milele; Bali ulimi wa uongo ni wa kitambo tu. Hila imo mioyoni mwao wafikirio uovu; Bali wafanyao mashauri ya amani, kwao kuna furaha. Mwenye haki hatapatikana na msiba wowote; Bali wasio haki watajazwa mabaya. Midomo ya uongo ni chukizo kwa BWANA; Bali watendao uaminifu ndio furaha yake. Mwanadamu mwenye busara husitiri maarifa; Bali moyo wa wapumbavu hutangaza upumbavu.

Soma Mithali 12