Methali 12:11-23
Methali 12:11-23 Biblia Habari Njema (BHN)
Mkulima mwenye bidii ana chakula tele, lakini afuataye mambo yasiyofaa hana akili. Waovu hutamani faida isiyo halali, lakini mtu mwadilifu husimama imara. Mtu mwovu hunaswa kwa uongo wake mwenyewe, lakini mwadilifu hutoka katika taabu. Mtu hufanikiwa kutokana na maneno yake kama apatavyo matokeo ya kazi za mikono yake. Mpumbavu huiona njia yake kuwa sawa, lakini mwenye hekima husikiliza shauri. Udhia wa mpumbavu hujulikana mara, lakini mwerevu huyapuuza matukano. Msema kweli hutoa ushahidi wa kweli, lakini shahidi wa uongo hutamka udanganyifu. Maneno ya ovyo hujeruhi kama upanga, lakini asemayo mwenye hekima huponesha kidonda. Ukweli hudumu milele, lakini uongo ni wa kitambo tu. Wanaopanga maovu wamejaa udanganyifu moyoni, lakini wanaonuia mema hupata furaha. Waadilifu hawapatwi na jambo lolote baya, lakini waovu wamejaa dhiki. Midomo isemayo uongo ni chukizo kwa Mwenyezi-Mungu, lakini watu waaminifu ni furaha yake. Mwenye busara huficha maarifa yake, lakini wapumbavu hutangaza upumbavu wao.
Methali 12:11-23 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Alimaye shamba lake atakuwa na chakula tele; Bali afuataye mambo ya upuzi hana ufahamu. Asiye haki hutamani nyavu za wabaya; Bali shina lao wenye haki huleta matunda. Katika kosa la midomo kuna mtego kwa mbaya; Bali mwenye haki atatoka katika taabu. Mtu atashiba mema kwa matunda ya kinywa chake; Na atarudishiwa matendo ya mikono yake. Njia ya mpumbavu imenyoka machoni pake mwenyewe; Bali yeye aliye na hekima husikiliza shauri. Ghadhabu ya mpumbavu hujulikana mara; Bali mtu mwerevu husitiri aibu. Atamkaye maneno ya kweli hufunua haki; Bali shahidi wa uongo hutamka hila. Kuna anenaye bila kufikiri, kama kuchoma kwa upanga; Bali ulimi wa mwenye haki ni afya. Mdomo wa kweli utathibitishwa milele; Bali ulimi wa uongo ni wa kitambo tu. Hila imo mioyoni mwao wafikirio uovu; Bali wafanyao mashauri ya amani, kwao kuna furaha. Mwenye haki hatapatikana na msiba wowote; Bali wasio haki watajazwa mabaya. Midomo ya uongo ni chukizo kwa BWANA; Bali watendao uaminifu ndio furaha yake. Mwanadamu mwenye busara husitiri maarifa; Bali moyo wa wapumbavu hutangaza upumbavu.
Methali 12:11-23 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Alimaye shamba lake atakuwa na chakula tele; Bali afuataye mambo ya upuzi hana ufahamu. Asiye haki hutamani nyavu za wabaya; Bali shina lao wenye haki huleta matunda. Katika kosa la midomo kuna mtego kwa mbaya; Bali mwenye haki atatoka katika taabu. Mtu atashiba mema kwa matunda ya kinywa chake; Na atarudishiwa matendo ya mikono yake. Njia ya mpumbavu imenyoka machoni pake mwenyewe; Bali yeye aliye na hekima husikiliza shauri. Ghadhabu ya mpumbavu hujulika mara; Bali mtu mwerevu husitiri aibu. Atamkaye maneno ya kweli hufunua haki; Bali shahidi wa uongo hutamka hila. Kuna anenaye bila kufikiri, kama kuchoma kwa upanga; Bali ulimi wa mwenye haki ni afya. Mdomo wa kweli utathibitishwa milele; Bali ulimi wa uongo ni wa kitambo tu. Hila imo mioyoni mwao wafikirio uovu; Bali wafanyao mashauri ya amani, kwao kuna furaha. Mwenye haki hatapatikana na msiba wo wote; Bali wasio haki watajazwa mabaya. Midomo ya uongo ni chukizo kwa BWANA; Bali watendao uaminifu ndio furaha yake. Mwanadamu mwenye busara husitiri maarifa; Bali moyo wa wapumbavu hutangaza upumbavu.
Methali 12:11-23 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Yeye alimaye shamba lake atakuwa na chakula tele, bali yeye afuataye mambo ya upuzi hana akili. Waovu hutamani mateka ya watu wabaya, bali shina la mwenye haki hustawi. Mtu mwovu hunaswa kwa mazungumzo yake ya dhambi, bali mwenye haki huepuka taabu. Kutokana na tunda la midomo yake mtu hujazwa na mambo mema, hakika kama ilivyo kazi ya mikono yake humtunza. Njia ya mpumbavu huonekana sawa machoni pake mwenyewe, bali mtu mwenye hekima husikiliza ushauri. Mpumbavu huonyesha kuudhika kwake mara moja, bali mtu wa busara hupuuza matukano. Shahidi wa kweli hutoa ushuhuda wa kuaminika, bali shahidi wa uongo husema uongo. Maneno ya kipumbavu huchoma kama upanga, bali ulimi wa mwenye hekima huleta uponyaji. Midomo isemayo kweli hudumu milele, bali ulimi wa uongo hudumu kwa muda mfupi tu. Upo udanganyifu katika mioyo ya wale ambao hupanga mabaya, bali kuna furaha kwa wale wanaoleta amani. Hakuna dhara linalompata mwenye haki, bali waovu wana taabu nyingi. BWANA anachukia sana midomo idanganyayo, bali hufurahia watu ambao ni wa kweli. Mtu mwenye busara hujihifadhia maarifa yeye mwenyewe, bali moyo wa wapumbavu hububujika upumbavu.