Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zab 69:30-36

Zab 69:30-36 SUV

Nitalisifu jina la Mungu kwa wimbo, Nami nitamtukuza kwa shukrani. Nayo yatampendeza BWANA kuliko ng’ombe, Au ndama mwenye pembe na kwato. Walioonewa watakapoona watafurahi; Enyi mmtafutao Mungu, mioyo yenu ihuishwe. Kwa kuwa BWANA huwasikia wahitaji, Wala hawadharau wafungwa wake. Mbingu na nchi zimsifu, Bahari na vyote viendavyo ndani yake. Maana Mungu ataiokoa Sayuni, na kuijenga miji ya Yuda, Na watu watakaa ndani yake na kuimiliki. Wazao wa watumishi wake watairithi, Nao walipendao jina lake watakaa humo.

Soma Zab 69

Mipango ya Kusoma Bila Malipo na Ibada zinazohusiana na Zab 69:30-36