Zaburi 69:30-36
Zaburi 69:30-36 Biblia Habari Njema (BHN)
Kwa wimbo nitalisifu jina la Mungu, nitamtukuza kwa shukrani. Jambo hili litampendeza Mwenyezi-Mungu zaidi, kuliko kumtolea tambiko ya ng'ombe, kuliko kumtolea fahali mzimamzima. Wanyonge wataona hayo na kufurahi; wanaomheshimu Mungu watapata moyo. Mwenyezi-Mungu huwasikiliza fukara; hatawasahau kamwe watu wake wafungwa. Enyi mbingu na dunia msifuni Mungu; bahari na vyote vilivyomo, msifuni. Maana Mungu atauokoa mji Siyoni, na kuijenga tena miji ya Yuda. Watu wake wataishi humo na kuimiliki; wazawa wa watumishi wake watairithi, wale wanaopenda jina lake wataishi humo.
Zaburi 69:30-36 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Nitalisifu jina la Mungu kwa wimbo, Nami nitamtukuza kwa shukrani. Nayo yatampendeza BWANA kuliko ng'ombe, Au ndama mwenye pembe na kwato. Walioonewa watakapoona watafurahi; Enyi mmtafutao Mungu, mioyo yenu ihuishwe. Kwa kuwa BWANA huwasikia wahitaji, Wala hawadharau wafungwa wake. Mbingu na nchi zimsifu, Bahari na vyote viendavyo ndani yake. Maana Mungu ataiokoa Sayuni, na kuijenga miji ya Yuda, Na watu watakaa ndani yake na kuimiliki. Wazawa wa watumishi wake watairithi, Nao walipendao jina lake watakaa humo.
Zaburi 69:30-36 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Nitalisifu jina la Mungu kwa wimbo, Nami nitamtukuza kwa shukrani. Nayo yatampendeza BWANA kuliko ng’ombe, Au ndama mwenye pembe na kwato. Walioonewa watakapoona watafurahi; Enyi mmtafutao Mungu, mioyo yenu ihuishwe. Kwa kuwa BWANA huwasikia wahitaji, Wala hawadharau wafungwa wake. Mbingu na nchi zimsifu, Bahari na vyote viendavyo ndani yake. Maana Mungu ataiokoa Sayuni, na kuijenga miji ya Yuda, Na watu watakaa ndani yake na kuimiliki. Wazao wa watumishi wake watairithi, Nao walipendao jina lake watakaa humo.
Zaburi 69:30-36 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Nitalisifu jina la Mungu kwa wimbo, nami nitamtukuza kwa kumtolea shukrani. Hili litampendeza BWANA kuliko ngʼombe dume, zaidi ya fahali akiwa na pembe na kwato zake. Maskini wataona na kufurahi: ninyi mnaomtafuta Mungu, mioyo yenu na iishi! BWANA huwasikia wahitaji wala hadharau watu wake waliotekwa. Mbingu na dunia zimsifu, bahari na vyote viendavyo ndani yake, kwa maana Mungu ataiokoa Sayuni na kuijenga tena miji ya Yuda. Kisha watu watafanya makao yao humo na kuimiliki, watoto wa watumishi wake watairithi na wale wote walipendao jina lake wataishi humo.