Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zaburi 69:30-36

Zaburi 69:30-36 SRUV

Nitalisifu jina la Mungu kwa wimbo, Nami nitamtukuza kwa shukrani. Nayo yatampendeza BWANA kuliko ng'ombe, Au ndama mwenye pembe na kwato. Walioonewa watakapoona watafurahi; Enyi mmtafutao Mungu, mioyo yenu ihuishwe. Kwa kuwa BWANA huwasikia wahitaji, Wala hawadharau wafungwa wake. Mbingu na nchi zimsifu, Bahari na vyote viendavyo ndani yake. Maana Mungu ataiokoa Sayuni, na kuijenga miji ya Yuda, Na watu watakaa ndani yake na kuimiliki. Wazawa wa watumishi wake watairithi, Nao walipendao jina lake watakaa humo.

Soma Zaburi 69

Mipango ya Kusoma Bila Malipo na Ibada zinazohusiana na Zaburi 69:30-36