Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zab 33:1-9

Zab 33:1-9 SUV

Mpigieni BWANA vigelegele, enyi wenye haki, Kusifu kunawapasa wanyofu wa moyo. Mshukuruni BWANA kwa kinubi, Kwa kinanda cha nyuzi kumi mwimbieni sifa. Mwimbieni wimbo mpya, Pigeni kwa ustadi kwa sauti ya shangwe. Kwa kuwa neno la BWANA lina adili, Na kazi yake yote huitenda kwa uaminifu. Huzipenda haki na hukumu, Nchi imejaa fadhili za BWANA. Kwa neno la BWANA mbingu zilifanyika, Na jeshi lake lote kwa pumzi ya kinywa chake. Hukusanya maji ya bahari chungu chungu, Huviweka vilindi katika ghala. Nchi yote na imwogope BWANA, Wote wakaao duniani na wamche. Maana Yeye alisema, ikawa; Na Yeye aliamuru, ikasimama.

Soma Zab 33

Mipango ya Kusoma Bila Malipo na Ibada zinazohusiana na Zab 33:1-9

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha