Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zab 33

33
Ukuu na Wema wa Mungu
1Mpigieni BWANA vigelegele, enyi wenye haki,
Kusifu kunawapasa wanyofu wa moyo.
2Mshukuruni BWANA kwa kinubi,
Kwa kinanda cha nyuzi kumi mwimbieni sifa.
3 # Isa 42:10 Mwimbieni wimbo mpya,
Pigeni kwa ustadi kwa sauti ya shangwe.
4Kwa kuwa neno la BWANA lina adili,
Na kazi yake yote huitenda kwa uaminifu.
5Huzipenda haki na hukumu,
Nchi imejaa fadhili za BWANA.
6 # Yn 1:1-3; Ebr 11:3; Ayu 26:13 Kwa neno la BWANA mbingu zilifanyika,
Na jeshi lake lote kwa pumzi ya kinywa chake.
7Hukusanya maji ya bahari chungu chungu,
Huviweka vilindi katika ghala.
8Nchi yote na imwogope BWANA,
Wote wakaao duniani na wamche.
9 # Mwa 1:3 Maana Yeye alisema, ikawa;
Na Yeye aliamuru, ikasimama.
10BWANA huyabatilisha mashauri ya mataifa,
Huyatangua makusudi ya watu.
11 # Ayu 23:13; Mit 19:21; Eze 38:10; Mdo 4:27,28 Shauri la BWANA lasimama milele,
Makusudi ya moyo wake vizazi na vizazi.
12Heri taifa ambalo BWANA ni Mungu wao,
Watu aliowachagua kuwa urithi wake.
13 # 2 Nya 16:9; Ayu 28:24; Zab 11:4 Toka mbinguni BWANA huchungulia,
Huwatazama wanadamu wote pia.
14Toka mahali pake aketipo
Huwaangalia wote wakaao duniani.
15 # Isa 64:8; Ayu 11:11; Zab 44:21; Mit 24:12; Yer 32:19; Hes 7:2 yeye aiumbaye mioyo yao wote
Huzifikiri kazi zao zote.
16Hapana mfalme aokokaye kwa wingi wa uwezo,
Wala shujaa haokoki kwa wingi wa nguvu.
17Farasi hafai kitu kwa wokovu,
Wala hamponyi mtu kwa wingi wa nguvu zake.
18 # Ayu 36:7; Zab 34:15 Tazama, jicho la BWANA li kwao wamchao,
Wazingojeao fadhili zake.
19Yeye huwaponya nafsi zao na mauti,
Na kuwahuisha wakati wa njaa.
20Nafsi zetu zinamngoja BWANA;
Yeye ndiye msaada wetu na ngao yetu.
21Maana mioyo yetu itamfurahia,
Kwa kuwa tumelitumainia jina lake takatifu.
22Ee BWANA, fadhili zako zikae nasi,
Kama vile tulivyokungoja Wewe.

Iliyochaguliwa sasa

Zab 33: SUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha