Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zaburi 33:1-9

Zaburi 33:1-9 SRUV

Mpigieni BWANA vigelegele, enyi wenye haki, Kusifu kunawapasa wanyofu wa moyo. Mshukuruni BWANA kwa kinubi, Kwa kinanda cha nyuzi kumi mwimbieni sifa. Mwimbieni wimbo mpya, Pigeni kwa ustadi kwa sauti ya shangwe. Kwa kuwa neno la BWANA lina adili, Na kazi yake yote huitenda kwa uaminifu. Huzipenda haki na hukumu, Nchi imejaa fadhili za BWANA. Kwa neno la BWANA mbingu ziliumbwa, Na jeshi lake lote kwa pumzi ya kinywa chake. Hukusanya maji ya bahari chungu chungu, Huviweka vilindi katika ghala. Nchi yote na imwogope BWANA, Wote wakaao duniani na wamche. Maana Yeye alisema, na ikawa; Na Yeye aliamuru, ikaumbika.

Soma Zaburi 33

Mipango ya Kusoma Bila Malipo na Ibada zinazohusiana na Zaburi 33:1-9

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha