Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zaburi 68:19-27

Zaburi 68:19-27 NENO

Ahimidiwe Bwana, Mungu Mwokozi wetu, ambaye siku kwa siku hutuchukulia mizigo yetu. Mungu wetu ni Mungu anayeokoa, Bwana Mungu Mwenyezi hutuokoa na kifo. Hakika Mungu ataponda vichwa vya adui zake, vichwa vya hao wanaoenda katika njia za dhambi. Bwana alisema, “Nitawarudisha kutoka Bashani; nitawarudisha kutoka vilindi vya bahari, ili uweze kuchovya miguu yako katika damu ya adui zako, huku ndimi za mbwa wako zikiwa na fungu lake.” Ee Mungu, maandamano yako yameonekana, maandamano ya Mungu wangu, Mfalme wangu, yakielekea patakatifu pake. Mbele wako waimbaji, baada yao wapiga vinanda, pamoja nao wako wanawali wakipiga matari. Msifuni Mungu katika kusanyiko kubwa, msifuni Mwenyezi Mungu katika kusanyiko la Israeli. Liko kabila dogo la Benyamini likiwaongoza, wakifuatwa na kundi kubwa la watawala wa Yuda, hatimaye watawala wa Zabuloni na Naftali.