Zaburi 68:19-27
Zaburi 68:19-27 Biblia Habari Njema (BHN)
Mwenyezi-Mungu asifiwe siku kwa siku! Yeye hutubebea mizigo yetu; yeye ndiye Mungu wa wokovu wetu. Mungu wetu ni Mungu mwenye kutuokoa; Bwana Mungu pekee ndiye aokoaye katika kifo. Mungu ataviponda vichwa vya maadui zake, naam, vichwa vya wanaoshikilia njia mbaya. Bwana alisema: “Nitawarudisha maadui kutoka Bashani; nitawarudisha kutoka vilindi vya bahari, uoshe miguu katika damu ya maadui zako, nao mbwa wako wale shibe yao.” Ee Mungu, misafara yako ya ushindi yaonekana; misafara ya Mungu wangu, mfalme wangu, hadi patakatifu pake! Mbele waimbaji, nyuma wanamuziki, katikati wasichana wanavumisha vigoma. “Msifuni Mungu katika jumuiya kubwa ya watu. Msifuni Mwenyezi-Mungu, enyi wazawa wa Israeli!” Kwanza ni Benyamini, mdogo wa wote; kisha viongozi wa Yuda na kundi lao, halafu wakuu wa Zebuluni na Naftali.
Zaburi 68:19-27 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Na ahimidiwe Bwana, Siku kwa siku hutuchukulia mzigo wetu; Mungu ndiye wokovu wetu. Mungu kwetu sisi ni Mungu wa kuokoa; Na njia za kutoka mautini zina YEHOVA Bwana. Naam, Mungu atakipasua kichwa cha adui zake, Utosi wenye nywele wa mtu afulizaye kukosa. Bwana alisema, Kutoka Bashani nitawarudisha, Nitawarudisha kutoka vilindi vya bahari; Uuchovye mguu wako katika damu ya adui zako, Na ulimi wa mbwa zako upate sehemu yake. Ee Mungu, wameiona miendo yako; Miendo ya Mungu wangu, Mfalme wangu, katika patakatifu Waimbaji hutangulia, nyuma yao wapigao vinanda, Kati ya wanawali wapiga matari. Mhimidini Mungu katika mikutano, Bwana katika makusanyiko ya Israeli. Yuko Benyamini mdogo, mtawala wao; Wakuu wa Yuda, kundi lao; Wakuu wa Zabuloni; Wakuu wa Naftali.

Zaburi 68:19-27 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Na ahimidiwe Bwana, Siku kwa siku hutuchukulia mzigo wetu; Mungu ndiye wokovu wetu. Mungu wetu ni Mungu wa kuokoa; Na njia za kutoka mautini zina YEHOVA Bwana. Naam, Mungu atakipasua kichwa cha adui zake, Utosi wenye nywele wa mtu afululizaye kukosa. Bwana alisema, Kutoka Bashani nitawarudisha, Nitawarudisha kutoka vilindi vya bahari; Uuchovye mguu wako katika damu ya adui zako, Na ulimi wa mbwa zako upate sehemu yake. Ee Mungu, wameiona miendo yako; Miendo ya Mungu wangu, Mfalme wangu, katika patakatifu. Waimbaji hutangulia, nyuma yao wapigao vinanda, Kati ya wanawali wapiga matari. Mhimidini Mungu katika mikutano, Bwana katika makusanyiko ya Israeli. Yuko Benyamini mdogo, mtawala wao; Wakuu wa Yuda, kundi lao; Wakuu wa Zabuloni; Wakuu wa Naftali.
Zaburi 68:19-27 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Na ahimidiwe Bwana, Siku kwa siku hutuchukulia mzigo wetu; Mungu ndiye wokovu wetu. Mungu kwetu sisi ni Mungu wa kuokoa; Na njia za kutoka mautini zina YEHOVA Bwana. Naam, Mungu atakipasua kichwa cha adui zake, Utosi wenye nywele wa mtu afulizaye kukosa. Bwana alisema, Kutoka Bashani nitawarudisha, Nitawarudisha kutoka vilindi vya bahari; Uuchovye mguu wako katika damu ya adui zako, Na ulimi wa mbwa zako upate sehemu yake. Ee Mungu, wameiona miendo yako; Miendo ya Mungu wangu, Mfalme wangu, katika patakatifu Waimbaji hutangulia, nyuma yao wapigao vinanda, Kati ya wanawali wapiga matari. Mhimidini Mungu katika mikutano, Bwana katika makusanyiko ya Israeli. Yuko Benyamini mdogo, mtawala wao; Wakuu wa Yuda, kundi lao; Wakuu wa Zabuloni; Wakuu wa Naftali.
Zaburi 68:19-27 Neno: Maandiko Matakatifu 2024 (NENO)
Ahimidiwe Bwana, Mungu Mwokozi wetu, ambaye siku kwa siku hutuchukulia mizigo yetu. Mungu wetu ni Mungu anayeokoa, Bwana Mungu Mwenyezi hutuokoa na kifo. Hakika Mungu ataponda vichwa vya adui zake, vichwa vya hao wanaoenda katika njia za dhambi. Bwana alisema, “Nitawarudisha kutoka Bashani; nitawarudisha kutoka vilindi vya bahari, ili uweze kuchovya miguu yako katika damu ya adui zako, huku ndimi za mbwa wako zikiwa na fungu lake.” Ee Mungu, maandamano yako yameonekana, maandamano ya Mungu wangu, Mfalme wangu, yakielekea patakatifu pake. Mbele wako waimbaji, baada yao wapiga vinanda, pamoja nao wako wanawali wakipiga matari. Msifuni Mungu katika kusanyiko kubwa, msifuni Mwenyezi Mungu katika kusanyiko la Israeli. Liko kabila dogo la Benyamini likiwaongoza, wakifuatwa na kundi kubwa la watawala wa Yuda, hatimaye watawala wa Zabuloni na Naftali.