Zab 68:19-27
![Zab 68:19-27 - Na ahimidiwe Bwana,
Siku kwa siku hutuchukulia mzigo wetu;
Mungu ndiye wokovu wetu.
Mungu kwetu sisi ni Mungu wa kuokoa;
Na njia za kutoka mautini zina YEHOVA Bwana.
Naam, Mungu atakipasua kichwa cha adui zake,
Utosi wenye nywele wa mtu afulizaye kukosa.
Bwana alisema, Kutoka Bashani nitawarudisha,
Nitawarudisha kutoka vilindi vya bahari;
Uuchovye mguu wako katika damu ya adui zako,
Na ulimi wa mbwa zako upate sehemu yake.
Ee Mungu, wameiona miendo yako;
Miendo ya Mungu wangu, Mfalme wangu, katika patakatifu
Waimbaji hutangulia, nyuma yao wapigao vinanda,
Kati ya wanawali wapiga matari.
Mhimidini Mungu katika mikutano,
Bwana katika makusanyiko ya Israeli.
Yuko Benyamini mdogo, mtawala wao;
Wakuu wa Yuda, kundi lao;
Wakuu wa Zabuloni;
Wakuu wa Naftali.](/_next/image?url=https%3A%2F%2Fimageproxy.youversionapi.com%2F320x320%2Fhttps%3A%2F%2Fs3.amazonaws.com%2Fstatic-youversionapi-com%2Fimages%2Fbase%2F6875%2F1280x1280.jpg&w=640&q=75)
Na ahimidiwe Bwana, Siku kwa siku hutuchukulia mzigo wetu; Mungu ndiye wokovu wetu. Mungu kwetu sisi ni Mungu wa kuokoa; Na njia za kutoka mautini zina YEHOVA Bwana. Naam, Mungu atakipasua kichwa cha adui zake, Utosi wenye nywele wa mtu afulizaye kukosa. Bwana alisema, Kutoka Bashani nitawarudisha, Nitawarudisha kutoka vilindi vya bahari; Uuchovye mguu wako katika damu ya adui zako, Na ulimi wa mbwa zako upate sehemu yake. Ee Mungu, wameiona miendo yako; Miendo ya Mungu wangu, Mfalme wangu, katika patakatifu Waimbaji hutangulia, nyuma yao wapigao vinanda, Kati ya wanawali wapiga matari. Mhimidini Mungu katika mikutano, Bwana katika makusanyiko ya Israeli. Yuko Benyamini mdogo, mtawala wao; Wakuu wa Yuda, kundi lao; Wakuu wa Zabuloni; Wakuu wa Naftali.
Zab 68:19-27