Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zaburi 17:1-5

Zaburi 17:1-5 NEN

Sikia, Ee BWANA, kusihi kwangu kwa haki, sikiliza kilio changu. Tega sikio kwa ombi langu, halitoki kwenye midomo ya udanganyifu. Hukumu yangu na itoke kwako, macho yako na yaone yale yaliyo haki. Ingawa unauchunguza moyo wangu na kunikagua usiku, ingawa umenijaribu, hutaona chochote. Nimeamua kwamba kinywa changu hakitatenda dhambi. Kuhusu matendo ya wanadamu: kwa neno la midomo yako, nimejiepusha na njia za wenye jeuri. Hatua zangu zimeshikamana na njia zako; nyayo zangu hazikuteleza.

Mipango ya Kusoma Bila Malipo na Ibada zinazohusiana na Zaburi 17:1-5