Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Mithali 8:10-19

Mithali 8:10-19 NEN

Chagua mafundisho yangu badala ya fedha, maarifa badala ya dhahabu safi, kwa maana hekima ina thamani kuliko marijani na hakuna chochote unachohitaji kinacholingana naye. “Mimi hekima, nakaa pamoja na busara; ninamiliki maarifa na busara. Kumcha BWANA ni kuchukia uovu; ninachukia kiburi na majivuno, tabia mbaya na mazungumzo potovu. Ushauri na hukumu sahihi ni vyangu; nina ufahamu na nina nguvu. Kwa msaada wangu wafalme hutawala na watawala hutunga sheria zilizo za haki, kwa msaada wangu wakuu hutawala, na wenye vyeo wote watawalao dunia. Nawapenda wale wanipendao, na wale wanitafutao kwa bidii wataniona. Utajiri na heshima viko kwangu, utajiri udumuo na mafanikio. Tunda langu ni bora kuliko dhahabu safi; kile nitoacho hupita fedha iliyo bora.

Mipango ya Kusoma Bila Malipo na Ibada zinazohusiana na Mithali 8:10-19