Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Methali 8:10-19

Methali 8:10-19 BHN

Chagua mafundisho yangu badala ya fedha; na maarifa badala ya dhahabu safi. “Mimi Hekima nina thamani kuliko johari; chochote unachotamani hakiwezi kulingana nami. Mimi Hekima ninao ujuzi; ninayo maarifa na busara. Kumcha Mwenyezi-Mungu ni kuchukia uovu. Nachukia kiburi, majivuno na maisha mabaya; nachukia na lugha mbaya. Nina uwezo wa kushauri na nina hekima. Ninao ujuzi na nina nguvu. Kwa msaada wangu wafalme hutawala, watawala huamua yaliyo ya haki. Kwa msaada wangu viongozi hutawala, wakuu na watawala halali. Nawapenda wale wanaonipenda; wanaonitafuta kwa bidii hunipata. Utajiri na heshima viko kwangu, mali ya kudumu na fanaka. Matunda yangu ni mazuri kuliko dhahabu safi, faida yangu yashinda ile ya fedha bora.

Soma Methali 8

Mipango ya Kusoma Bila Malipo na Ibada zinazohusiana na Methali 8:10-19