Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Mithali 8:10-19

Mithali 8:10-19 SRUV

Pokea mafundisho yangu, wala si fedha, Na maarifa kuliko dhahabu safi. Maana hekima ni bora kuliko marijani; Wala vyote vinavyotamanika havilingani nayo. Mimi, hekima, nimefanya werevu kuwa makao yangu; Natafuta maarifa na busara. Kumcha BWANA ni kuchukia uovu; Kiburi na majivuno, na njia mbovu, Na kinywa cha ukaidi pia nakichukia. Ushauri ni wangu, na maarifa yaliyo sahihi; Mimi ni ufahamu, mimi nina nguvu. Kwa msaada wangu wafalme humiliki, Na wakuu wanahukumu haki. Kwa msaada wangu wakuu hutawala, Na waungwana, naam, waamuzi wote wa dunia. Nawapenda wale wanipendao, Na wale wanitafutao kwa bidii wataniona. Utajiri na heshima ziko kwangu, Naam, utajiri udumuo, na haki pia. Matunda yangu ni bora kuliko dhahabu, naam, dhahabu safi, Na faida yangu ni bora kuliko fedha iliyo safi.

Soma Mithali 8

Mipango ya Kusoma Bila Malipo na Ibada zinazohusiana na Mithali 8:10-19