Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Ezra 2

2
Orodha ya watu waliorudi kutoka uhamishoni
(Nehemia 7:4-73)
1Basi hawa ndio watu wa jimbo waliotoka uhamishoni, ambao Nebukadneza mfalme wa Babeli alikuwa amewachukua mateka hadi Babeli (walirudi Yerusalemu na Yuda, kila mmoja kwenye mji wake, 2wakiwa wamefuatana na Zerubabeli, Yeshua, Nehemia, Seraya, Reelaya, Mordekai, Bilshani, Mispari, Bigwai, Rehumu na Baana):
Orodha ya wanaume kati ya watu wa Israeli ilikuwa:
3wazao wa Paroshi, elfu mbili mia moja sabini na wawili (2,172);
4wazao wa Shefatia, mia tatu sabini na wawili (372);
5wazao wa Ara, mia saba sabini na watano (775);
6wazao wa Pahath-Moabu (wa jamaa ya Yeshua na Yoabu), elfu mbili mia nane na kumi na wawili (2,812);
7wazao wa Elamu, elfu moja mia mbili hamsini na wanne (1,254);
8wazao wa Zatu, mia tisa arobaini na watano (945);
9wazao wa Zakai, mia saba na sitini (760);
10wazao wa Bani, mia sita arobaini na wawili (642);
11wazao wa Bebai, mia sita ishirini na watatu (623);
12wazao wa Azgadi, elfu moja mia mbili ishirini na wawili (1,222);
13wazao wa Adonikamu, mia sita sitini na sita (666);
14wazao wa Bigwai, elfu mbili hamsini na sita (2,056);
15wazao wa Adini, mia nne hamsini na wanne (454);
16wazao wa Ateri (kupitia Hezekia), tisini na nane (98);
17wazao wa Besai, mia tatu ishirini na watatu (323);
18wazao wa Yora, mia moja na kumi na wawili (112);
19wazao wa Hashumu, mia mbili na ishirini na watatu (223);
20wazao wa Gibari, tisini na watano (95);
21watu wa Bethlehemu, mia moja ishirini na watatu (123);
22watu wa Netofa, hamsini na sita (56);
23watu wa Anathothi, watu mia moja ishirini na nane (128);
24watu wa Azmawethi, arobaini na wawili (42);
25wazao wa Kiriath-Yearimu, Kefira na Beerothi, mia saba arobaini na watatu (743);
26wazao wa Rama na Geba, mia sita ishirini na mmoja (621);
27watu wa Mikmashi, mia moja ishirini na wawili (122);
28watu wa Betheli na Ai, mia mbili na ishirini na watatu (223);
29wazao wa Nebo, hamsini na wawili (52);
30wazao wa Magbishi, mia moja hamsini na sita (156);
31wazao wa Elamu ile ingine, elfu moja mia mbili hamsini na wanne (1,254);
32wazao wa Harimu, mia tatu na ishirini (320);
33wazao wa Lodi, Hadidi na Ono, mia saba ishirini na watano (725);
34wazao wa Yeriko, mia tatu arobaini na watano (345);
35wazao wa Senaa, elfu tatu mia sita na thelathini (3,630).
36Makuhani:
wazao wa Yedaya (kwa jamaa ya Yeshua), mia tisa sabini na watatu (973);
37wazao wa Imeri, elfu moja hamsini na wawili (1,052);
38wazao wa Pashuri, elfu moja mia mbili arobaini na saba (1,247);
39wazao wa Harimu, elfu moja na kumi na saba (1,017).
40Walawi:
wazao wa Yeshua na Kadmieli (kupitia jamaa ya Hodavia), sabini na wanne (74).
41Waimbaji:
wazao wa Asafu, mia moja ishirini na nane (128).
42Mabawabu wa lango la Hekalu:
wazao wa Shalumu, Ateri, Talmoni, Akubu, Hatita na Shobai, mia moja thelathini na tisa (139).
43Watumishi wa Hekalu#2:43 yaani Wanethini (pia 2:58, 70).:
wazao wa Siha, Hasufa, Tabaothi,
44wazao wa Kerosi, Siaha, Padoni,
45wazao wa Lebana, Hagaba, Akubu,
46wazao wa Hagabu, Shalmai, Hanani,
47wazao wa Gideli, Gahari, Reaya,
48wazao wa Resini, Nekoda, Gazamu,
49wazao wa Uza, Pasea, Besai,
50wazao wa Asna, Meunimu, Nefusimu,
51wazao wa Bakbuki, Hakufa, Harhuri,
52wazao wa Basluthi, Mehida, Harsha,
53wazao wa Barkosi, Sisera, Tema,
54wazao wa Nesia na Hatifa.
55Wazao wa watumishi wa Sulemani:
wazao wa Sotai, Hasaferethi, Peruda,
56wazao wa Yaala, Darkoni, Gideli,
57wazao wa Shefatia, Hatili, Pokereth-Hasebaimu na Ami.
58Watumishi wa Hekalu, na wazao wa watumishi wa Sulemani, mia tatu tisini na wawili (392).
59Wafuatao walikuja kutoka miji ya Tel-Mela, Tel-Harsha, Kerubu, Adoni na Imeri, lakini hawakuweza kuthibitisha kwamba jamaa zao zilikuwa uzao wa Israeli:
60wazao wa Delaya, Tobia na Nekoda, mia sita hamsini na wawili (652).
61Kutoka miongoni mwa makuhani:
Wazao wa Hobaya, Hakosi, Barzilai (mtu aliyemwoa binti Barzilai Mgileadi, naye akaitwa kwa jina hilo).
62Hawa walitafuta orodha za jamaa zao, lakini hawakuonekana humo, kwa hiyo waliondolewa ukuhani kwa kuwa walihesabiwa kuwa najisi. 63Mtawala aliagiza kuwa wasile chochote miongoni mwa vyakula vitakatifu hadi kuwe kuhani atakayehudumu kwa Urimu na Thumimu#2:63 Urimu na Thumimu maana yake ni Nuru na Kweli; vifaa hivi viliwekwa kwenye kifuko cha kifuani cha kisibau cha kuhani mkuu ili kujua mapenzi ya Mungu kwenye mambo ya kutatanisha..
64Jumla ya watu wote waliorudi walikuwa elfu arobaini na mbili na mia tatu na sitini (42,360); 65tena zaidi ya hao walikuwa na watumwa wa kiume na wa kike elfu saba, mia tatu na thelathini na saba (7,337); pia walikuwa na waimbaji wanaume na wanawake mia mbili. 66Walikuwa na farasi mia saba thelathini na sita (736), nyumbu mia mbili arobaini na watano (245), 67ngamia mia nne thelathini na watano (435), na punda elfu sita, mia saba na ishirini (6,720).
68Walipofika kwenye nyumba ya Mwenyezi Mungu huko Yerusalemu, baadhi ya viongozi wa jamaa walitoa sadaka za hiari kwa ajili ya kujenga upya nyumba ya Mungu katika eneo lake. 69Wakatoa kwa kadiri ya uwezo wao na kutia katika hazina darkoni elfu sitini na moja#2:69 Darkoni 61,000 za dhahabu ni sawa na kilo 500. za dhahabu, mane elfu tano#2:69 Mane 5,000 za fedha ni sawa na kilo 2,900. za fedha, na mavazi mia moja ya ukuhani kwa ajili ya kazi hiyo.
70Makuhani, Walawi, waimbaji, mabawabu, na watumishi wa Hekalu waliishi katika miji yao wenyewe, pamoja na baadhi ya watu wengine, nao Waisraeli waliosalia waliishi katika miji yao.

Iliyochaguliwa sasa

Ezra 2: NENO

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia