Walipofika kwenye nyumba ya Mwenyezi Mungu huko Yerusalemu, baadhi ya viongozi wa jamaa walitoa sadaka za hiari kwa ajili ya kujenga upya nyumba ya Mungu katika eneo lake. Wakatoa kwa kadiri ya uwezo wao na kutia katika hazina darkoni elfu sitini na moja za dhahabu, mane elfu tano za fedha, na mavazi mia moja ya ukuhani kwa ajili ya kazi hiyo.