“Hili ndilo asemalo Koreshi mfalme wa Uajemi:
“ ‘Mwenyezi Mungu, Mungu wa mbinguni, amenipa falme zote duniani, na ameniagiza kumjengea Hekalu huko Yerusalemu katika Yuda. Yeyote kati ya watu wa Mungu miongoni mwenu, Mungu wake na awe pamoja naye, wacha apande kwenda Yerusalemu katika Yuda na kujenga Hekalu la Mwenyezi Mungu, Mungu wa Israeli, Mungu aliyeko Yerusalemu.