Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Ezra 1

1
Koreshi aruhusu watu kurudi Yerusalemu
(2 Nyakati 36:22-23)
1Katika mwaka wa kwanza wa utawala wa Koreshi mfalme wa Uajemi, ili kulitimiza neno la Mwenyezi Mungu lililosemwa na nabii Yeremia, Mwenyezi Mungu aliusukuma moyo wa Koreshi mfalme wa Uajemi kutangaza katika himaya yake yote kwa maandishi:
2“Hili ndilo asemalo Koreshi mfalme wa Uajemi:
“ ‘Mwenyezi Mungu, Mungu wa mbinguni, amenipa falme zote duniani, na ameniagiza kumjengea Hekalu huko Yerusalemu katika Yuda. 3Yeyote kati ya watu wa Mungu miongoni mwenu, Mungu wake na awe pamoja naye, wacha apande kwenda Yerusalemu katika Yuda na kujenga Hekalu la Mwenyezi Mungu, Mungu wa Israeli, Mungu aliyeko Yerusalemu. 4Nao wakazi wa popote manusura wanapoishi sasa, wawape manusura fedha na dhahabu, pamoja na vifaa na mifugo, na sadaka za hiari kwa ajili ya Hekalu la Mungu huko Yerusalemu.’ ”
5Kisha viongozi wa jamaa ya Yuda na Benyamini na makuhani na Walawi kila mmoja ambaye moyo wake ulisukumwa na Mungu, akajiandaa kupanda ili kuijenga nyumba ya Mwenyezi Mungu huko Yerusalemu. 6Majirani zao wote wakawasaidia vyombo vya fedha na dhahabu, pamoja na vifaa na mifugo, pia na zawadi za thamani, pamoja na sadaka zote za hiari. 7Zaidi ya hayo, Mfalme Koreshi akavitoa vyombo vilivyokuwa mali ya Hekalu la Mwenyezi Mungu, ambavyo Nebukadneza alikuwa amevichukua kutoka Yerusalemu na kuviweka katika hekalu la mungu wake. 8Koreshi mfalme wa Uajemi akavitoa kwa mkono wa Mithredathi mtunza hazina, aliyevihesabu mbele ya Sheshbaza mkuu wa Yuda.
9Hii ilikuwa orodha ya vifaa:
masinia ya dhahabu yalikuwa thelathini;
masinia ya fedha yalikuwa elfu moja;
vyetezo vya fedha vilikuwa ishirini na tisa;
10mabakuli ya dhahabu yalikuwa thelathini;
mabakuli ya fedha yaliyofanana yalikuwa mia nne na kumi;
vifaa vingine vilikuwa elfu moja.
11Kwa jumla, kulikuwa na vyombo elfu tano na mia nne vya dhahabu na vya fedha.
Sheshbaza akavileta hivi vyote wakati watu walipotoka uhamishoni Babeli kwenda Yerusalemu.

Iliyochaguliwa sasa

Ezra 1: NENO

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia