Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Ezra Utangulizi

Utangulizi
Vitabu vya Ezra na Nehemia vilikuwa kitabu kimoja katika Maandiko Matakatifu ya Kiebrania ambacho kilijulikana kama Ezra. Kitabu cha Ezra kinaeleza kuhusu kurudi kwa Wayahudi kutoka uhamishoni Babeli. Kinaanzia 539 K.K. na agizo alilotoa Koreshi, mfalme wa Uajemi, kwamba Waisraeli warudi Yerusalemu chini ya uongozi wa Zerubabeli. Agizo hili limetajwa katika milango miwili ya mwisho ya Mambo ya Nyakati. Watu walianza kujenga Hekalu kwa shauku na juhudi kubwa, na wakaanza kutoa dhabihu. Lakini kwa miaka 18 walicheleweshwa na adui zao kutoka kaskazini. Hatimaye mnamo 521 K.K. agizo kutoka kwa Dario mfalme wa Uajemi liliwapa nafasi ya kumalizia ujenzi huo. Walikamilisha kazi hiyo na kuweka Hekalu wakfu mnamo 516 K.K.
Katika mwaka wa 458 K.K., Kuhani Ezra aliwasili Yerusalemu akiwa na kundi jingine la watu waliokuwa wamesalia uhamishoni huko Babeli. Aliwafundisha watu Torati ya Musa, na akarekebisha maisha yao ya kiroho ili mataifa yaliyowazunguka waweze kuona kwamba hili ni taifa lililochaguliwa na Mwenyezi Mungu.
Mwandishi
Inadhaniwa kwamba Ezra aliandika kitabu hiki.
Kusudi
Kuonesha uaminifu wa Mwenyezi Mungu, na jinsi alivyotimiza ahadi yake kwa kuwarejesha watu wake katika nchi yao.
Mahali
Babeli na Yerusalemu.
Tarehe
Kama mwaka wa 450 K.K.
Wahusika Wakuu
Koreshi, Zerubabeli, Hagai, Zekaria, Dario wa Kwanza, Artashasta wa Kwanza, na Ezra.
Wazo Kuu
Kuweka kumbukumbu ya mkusanyiko wa kwanza wa Israeli kitaifa baada ya kutawanyika miongoni mwa mataifa; pia kuonesha matatizo yanayoambatana na uhamisho wa kidini kuwiana na Torati ya Musa.
Mambo Muhimu
Kurudi kwa Wayahudi kutoka uhamishoni; kujengwa upya kwa Hekalu; matatizo yaliyowakabili Waisraeli kutokana na kulijenga Hekalu tena.
Yaliyomo
Watu wa kwanza kutoka uhamishoni Babeli na kurudi Yuda (1:1–2:70)
Kujengwa kwa Hekalu na upinzani (3:1–6:22)
Ezra arudi na kikundi cha pili kutoka Babeli, na marekebisho yake (7:1–10:44).

Iliyochaguliwa sasa

Ezra Utangulizi: NENO

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia