2 Timotheo 4:7-8
2 Timotheo 4:7-8 NEN
Nimevipiga vita vizuri, mashindano nimeyamaliza, imani nimeilinda. Sasa nimewekewa taji ya haki ambayo Bwana, mwamuzi wa haki, atanitunukia siku ile: wala si mimi tu, bali pia wote ambao wamengoja kwa shauku kudhihirishwa kwake.