Lakini huyo mwanamke akapewa mabawa mawili ya tai mkubwa, kusudi aweze kuruka hadi mahali palipotayarishwa kwa ajili yake huko jangwani, ambako atatunzwa kwa wakati na nyakati na nusu, ya wakati ambako lile joka haliwezi kufika. Ndipo lile joka likamwaga maji kama mto kutoka kinywani mwake, ili kumfikia huyo mwanamke, achukuliwe na mafuriko. Lakini nchi ikamsaidia huyo mwanamke kwa kufungua kinywa na kuumeza huo mto ambao lile joka lilikuwa limeutoa kinywani mwake.