1
Isaya 53:5
Neno: Maandiko Matakatifu 2024
Lakini alijeruhiwa kwa ajili ya makosa yetu, alichubuliwa kwa ajili ya maovu yetu; adhabu iliyotuletea sisi amani ilikuwa juu yake, na kwa majeraha yake sisi tumepona.
Linganisha
Chunguza Isaya 53:5
2
Isaya 53:6
Sisi sote, kama kondoo, tumepotea, kila mmoja wetu amegeukia njia yake mwenyewe, naye Mwenyezi Mungu aliweka juu yake maovu yetu sisi sote.
Chunguza Isaya 53:6
3
Isaya 53:4
Hakika alichukua udhaifu wetu na akajitwika huzuni zetu; tulidhania kuwa ameadhibiwa na Mungu, naye akapigwa sana na kujeruhiwa.
Chunguza Isaya 53:4
4
Isaya 53:3
Alidharauliwa na kukataliwa na wanadamu, mtu wa huzuni nyingi, ajuaye mateso. Kama mtu ambaye watu humficha nyuso zao, alidharauliwa, wala hatukumhesabu kuwa kitu.
Chunguza Isaya 53:3
5
Isaya 53:7
Alionewa na kuteswa, hata hivyo hakufungua kinywa chake; aliongozwa kama mwana-kondoo apelekwaye machinjoni, kama vile kondoo anyamazavyo mbele ya wao wamkataye manyoya, hivyo hakufungua kinywa chake.
Chunguza Isaya 53:7
6
Isaya 53:10
Lakini yalikuwa ni mapenzi ya Mwenyezi Mungu kumchubua na kumsababisha ateseke. Ingawa Mwenyezi Mungu amefanya maisha yake kuwa sadaka ya hatia, ataona uzao wake na kuishi siku nyingi, nayo mapenzi ya Mwenyezi Mungu yatafanikiwa mkononi mwake.
Chunguza Isaya 53:10
7
Isaya 53:2
Alikua mbele yake kama mche mwororo na kama mzizi katika nchi kavu. Hakuwa na uzuri wala utukufu wa kutuvutia kwake, hakuwa na chochote katika sura yake cha kutufanya tumtamani.
Chunguza Isaya 53:2
8
Isaya 53:12
Kwa hiyo nitamgawia sehemu miongoni mwa wakuu, naye atagawana nyara pamoja na wenye nguvu, kwa sababu aliyamimina maisha yake hadi mauti, naye alihesabiwa pamoja na wakosaji. Kwa kuwa alichukua dhambi za wengi, na kuwaombea wakosaji.
Chunguza Isaya 53:12
9
Isaya 53:11
Baada ya maumivu ya nafsi yake, ataona nuru ya uzima na kuridhika; kwa maarifa yake, mtumishi wangu mwenye haki atawafanya wengi kuwa wenye haki, naye atayachukua maovu yao.
Chunguza Isaya 53:11
10
Isaya 53:8
Kwa kuonewa na kuhukumiwa aliondolewa. Nani awezaye kueleza kuhusu kizazi chake? Kwa maana alikatiliwa mbali na nchi ya walio hai, alipigwa kwa ajili ya makosa ya watu wangu.
Chunguza Isaya 53:8
11
Isaya 53:9
Wakamfanyia kaburi pamoja na waovu, pamoja na matajiri katika kifo chake, ingawa hakutenda jeuri, wala hapakuwa na hila kinywani mwake.
Chunguza Isaya 53:9
Nyumbani
Bibilia
Mipango
Video