Kila mwanaume kifungua mimba katika Misri atakufa, kuanzia mzaliwa wa kwanza wa kiume wa Farao, anayeketi kwenye kiti cha ufalme, hadi mzaliwa wa kwanza wa kiume wa mjakazi, anayesaga nafaka kwa jiwe, pamoja na kila mzaliwa wa kwanza wa mifugo. Kutakuwa na kilio kikubwa katika nchi yote ya Misri, kilio ambacho hakijakuwa, wala kamwe hakitakuwa tena.