Watoto wenu watakapowauliza, ‘Sikukuu hii ina maana gani kwenu?’ Basi waambieni, ‘Hii ni dhabihu ya Pasaka kwa Mwenyezi Mungu, ambaye alipita juu ya nyumba za Waisraeli katika nchi ya Misri, na hakudhuru nyumba zetu alipowapiga Wamisri.’ ” Ndipo Waisraeli walisujudu na kuabudu.