1
Kutoka 13:21-22
Neno: Maandiko Matakatifu 2024
Wakati wa mchana Mwenyezi Mungu aliwatangulia kwa nguzo ya wingu kuwaongoza katika njia yao, na wakati wa usiku aliwatangulia kwa nguzo ya moto kuwaangazia, ili waweze kusafiri mchana au usiku. Ile nguzo ya wingu wakati wa mchana au ile nguzo ya moto wakati wa usiku haikuondoka mahali pake mbele ya watu.
Linganisha
Chunguza Kutoka 13:21-22
2
Kutoka 13:17
Farao alipowaachia watu waende, Mungu hakuwaongoza kufuata njia ipitayo katika nchi ya Wafilisti, ingawa njia hiyo ilikuwa fupi zaidi. Kwa maana Mungu alisema, “Wakikabiliana na vita, wanaweza kubadili mawazo yao na kurudi Misri.”
Chunguza Kutoka 13:17
3
Kutoka 13:18
Kwa hiyo Mungu akawaongoza watu kupitia njia ya kuzunguka kupitia jangwani, kuelekea Bahari ya Shamu. Waisraeli walipanda kutoka nchi ya Misri wakiwa wamejiandaa kwa vita.
Chunguza Kutoka 13:18
Nyumbani
Bibilia
Mipango
Video