1
Kumbukumbu 28:1
Neno: Maandiko Matakatifu 2024
Ukimtii Mwenyezi Mungu, Mungu wako, kwa ukamilifu na kufuata amri zake zote ninazokupa leo kwa makini, Mwenyezi Mungu, Mungu wako, atakuweka juu ya mataifa yote katika dunia.
Linganisha
Chunguza Kumbukumbu 28:1
2
Kumbukumbu 28:2
Baraka hizi zote zitakuja juu yako na kukupata, kama ukimtii Mwenyezi Mungu, Mungu wako
Chunguza Kumbukumbu 28:2
3
Kumbukumbu 28:13
Mwenyezi Mungu atakufanya kichwa, wala si mkia. Kama utazingatia maagizo ya Mwenyezi Mungu, Mungu wako, ninayokupa siku hii ya leo na kuyafuata kwa makini, daima utakuwa juu, kamwe hutakuwa chini.
Chunguza Kumbukumbu 28:13
4
Kumbukumbu 28:12
Mwenyezi Mungu atafungua mbingu, ghala zake za baraka, kukupa mvua kwa majira yake na kubariki kazi zako zote za mikono yako. Utakopesha mataifa mengi lakini hutakopa kwa yeyote.
Chunguza Kumbukumbu 28:12
5
Kumbukumbu 28:7
Mwenyezi Mungu atasababisha adui wainukao dhidi yako kushindwa mbele yako. Watakujia kwa njia moja lakini watakimbia mbele yako kwa njia saba.
Chunguza Kumbukumbu 28:7
6
Kumbukumbu 28:8
Mwenyezi Mungu ataagiza baraka juu ya ghala zako na juu ya kila kitu utakachogusa kwa mkono wako. Mwenyezi Mungu, Mungu wako, atakubariki katika nchi anayokupa.
Chunguza Kumbukumbu 28:8
7
Kumbukumbu 28:6
Utabarikiwa uingiapo na utabarikiwa utokapo.
Chunguza Kumbukumbu 28:6
8
Kumbukumbu 28:3
Utabarikiwa mjini na utabarikiwa mashambani.
Chunguza Kumbukumbu 28:3
9
Kumbukumbu 28:4
Utabarikiwa uzao wa tumbo lako, na mazao ya nchi yako na mifugo wako wachanga, yaani ndama wa makundi yako ya ng’ombe, na wana-kondoo wa makundi yako.
Chunguza Kumbukumbu 28:4
10
Kumbukumbu 28:9
Mwenyezi Mungu atakufanya kuwa taifa lake takatifu, kama alivyokuahidi kwa kiapo, ukishika maagizo ya Mwenyezi Mungu, Mungu wako, na kwenda katika njia zake.
Chunguza Kumbukumbu 28:9
11
Kumbukumbu 28:5
Kapu lako na vyombo vyako vya kukandia vitabarikiwa.
Chunguza Kumbukumbu 28:5
12
Kumbukumbu 28:11
Mwenyezi Mungu atakupa kustawi kwa wingi, katika tunda la uzao wa tumbo lako, katika wanyama wachanga wa mifugo yako na katika mazao ya ardhi yako, katika nchi aliyowaapia baba zako kukupa wewe.
Chunguza Kumbukumbu 28:11
13
Kumbukumbu 28:10
Kisha mataifa yote ya dunia wataona kuwa unaitwa kwa jina la Mwenyezi Mungu, nao watakuogopa.
Chunguza Kumbukumbu 28:10
14
Kumbukumbu 28:14
Usihalifu amri zangu zozote ninazokupa leo, kwa kwenda kuume au kushoto, kwa kufuata miungu mingine na kuitumikia.
Chunguza Kumbukumbu 28:14
15
Kumbukumbu 28:15
Lakini kama hutamtii Mwenyezi Mungu, Mungu wako, na kuzishika kwa makini amri zake zote na maagizo ninayokupa leo, laana hizi zote zitakuja juu yako na kukupata
Chunguza Kumbukumbu 28:15
Nyumbani
Bibilia
Mipango
Video