YouVersion Logo
Search Icon

Soma Biblia Kila Siku/AGOSTI 2023Sample

Soma Biblia Kila Siku/AGOSTI 2023

DAY 27 OF 31

Daudi anaanza na mwaliko kwa watu wa Mungu, waungane naye katika kumpa Mungu utukufu na kumfanyia ibada, maana ndiye mfalme milele. Yote anayoyatenda yana kusudi la Mungu kujitambulisha kwa watu wake ili wamwabudu na kumtegemea. Hali ya msitu uliovurugwa na ghasia inamwacha Daudi katika kumbukumbu la utukufu na nguvu ya Mungu isiyoweza kuzuilika. Habari zote zinashuhudia utukufu wa Mwenyezi Mungu. Yuko tayari kuwabariki watu wake, akiwapa amani na nguvu. Je, ni mfalme pia katika maisha yako?

Day 26Day 28

About this Plan

Soma Biblia Kila Siku/AGOSTI 2023

Soma Biblia Kila Siku Agosti 2023 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kuelewa somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu Yohana na Mithali. Karibu kujiunga na mpango huu.

More