YouVersion Logo
Search Icon

Soma Biblia Kila Siku/AGOSTI 2023Sample

Soma Biblia Kila Siku/AGOSTI 2023

DAY 25 OF 31

Yesu alipoiona huzuni ya Mariamu na wale waliokuja kumfariji akaugua rohoni mwake akalia machozi (ukipenda rudia m.33-36)! Akamwomba Baba yake amfufue Lazaro (m.41-42,Baba, nakushukuru kwa kuwa umenisikia. Nami nalijua ya kuwa wewe wanisikia sikuzote).Naye akiisha kusema hayo, akalia kwa sauti kuu, Lazaro, njoo huku nje. Akatoka nje yule aliyekufa, amefungwa sanda miguuni na mikononi(m.43-44). Ajabu sana, sivyo? Aliyetenda haya ni NENO ambaye vituvyote vilifanyika kwa huyo; wala pasipo yeye hakikufanyika cho chote kilichofanyika(Yn 1:1-3)! Kwa ishara hii Yesu alitukuzwa. Inathibitisha pia ukweli wa maneno yake aliyosema:Mimi ndimi ufufuo na uzima!

Scripture

Day 24Day 26

About this Plan

Soma Biblia Kila Siku/AGOSTI 2023

Soma Biblia Kila Siku Agosti 2023 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kuelewa somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu Yohana na Mithali. Karibu kujiunga na mpango huu.

More