BibleProject | Tafakari ya Ujio wa YesuSample

Mtume Paulo anasema kuwa Yesu mwenyewe ndiye amani yetu. Yesu aliondoa vitu vyote vinavyowatenga wanadamu kutoka miongoni mwao na kutoka kwa Mungu na sasa anatoa amani yake kwa wengine kama zawadi. Wafuasi wa Yesu wameitwa kupokea, kutunza na kukuza zawadi hii ya amani, inayohitaji unyenyekevu, upole, subira, na upendo.
Soma:
Waefeso 2:11-15, Waefeso 4:1-3, Waefeso 4:29-32
Tafakari:
Kwa mujibu wa kifungu hiki, Yesu aliletaje amani kati ya vikundi viwili vilivyotengana kabisa (Wayahudi na Watu wa Mataifa), na ni kwa nini alifanya hivyo (tazama mstari wa 2:16)?
Je, unahisi umetengwa kutoka kwa mtu yeyote katika maisha yako? Je, unataka kufurahia amani na mtu huyu tena? Kwa nini au kwa nini hutaki? Jaribu kuzingatia kile ambacho Yesu alikifanya ili kuleta amani. Ni maswali na hisia zipi zinajitokeza unavyotafakari kuhusu hili?
Chambua Waefeso 4:1-3 kwa makini. Unafikiri unyenyekevu, upole, subira na upendo husaidia vipi kudumisha umoja ambao Yesu alileta kwa wafuasi wake? Ni nini hutokea mojawapo ya maadili haya yanapokosekana? Huwezi kuwaamulia wengine, lakini ni uamuzi upi mmoja halisi unaoweza kufanya leo ili kukuza amani?
Chambua Waefeso 4:29-32 kwa kina. Yesu amekusamehe vipi? Je ni nani anahitaji msamaha wako?
About this Plan

BibleProject ilibuni Tafakari ya Ujio wa Yesu ili kuhamasisha watu mmoja mmoja, vikundi vidogo vidogo, na familia kusherehekea majilio, au kuwasili kwa Yesu. Mwongozo huu wa wiki nne unashirikisha video za kikatuni, mihutasari mifupi, na maswali ya kutafakari ili kuwasaidia washiriki kuchunguza maana ya Biblia ya tumaini, amani, furaha, na upendo. Chagua mwongozo huu ili kujifunza jinsi maadili haya manne yamefika ulimwenguni kupitia kwa Yesu.
More
Related Plans

You Are Not Alone.

God in the Midst of Depression

Ready as You Are

Leading With Faith in the Hard Places

Church Planting in the Book of Acts

EquipHer Vol. 12: "From Success to Significance"

BibleProject | Sermon on the Mount

Acts 10:9-33 | When God Has a New Way

7-Day Devotional: Torn Between Two Worlds – Embracing God’s Gifts Amid Unmet Longings
