BibleProject | Tafakari ya Ujio wa YesuSample
Waisraeli walichagua njia yao wenyewe mbali na Mungu. Kwa sababu hiyo, walifukuzwa kutoka katika nchi yao na kutawalwa na mataifa ya kigeni. Lakini nabii Isaya alijua kuwa huzuni na majonzi hayatadumu milele. Alitazamia siku ambayo Mungu wa Israeli mwenye neema angeinua mkombozi ili kuwakomboa kutoka katika ukandamizaji na kuwaongoza hadi kwenye furaha ya milele.
Soma:
Isaya 51:11, Isaya 49:13
Tafakari:
Tambua maeneo ya maisha yako yanayokusababishia uzito na ukakasi sasa hivi.
Chambua vifungu vya leo polepole ukizingatia uzoefu wako wa msiba au huzuni. Ni mawazo au hisia zipi zinaibuka unavyosoma tena?
Omba Mungu akufariji kwa mtazamo mpya wa furaha yake ya milele.
Scripture
About this Plan
BibleProject ilibuni Tafakari ya Ujio wa Yesu ili kuhamasisha watu mmoja mmoja, vikundi vidogo vidogo, na familia kusherehekea majilio, au kuwasili kwa Yesu. Mwongozo huu wa wiki nne unashirikisha video za kikatuni, mihutasari mifupi, na maswali ya kutafakari ili kuwasaidia washiriki kuchunguza maana ya Biblia ya tumaini, amani, furaha, na upendo. Chagua mwongozo huu ili kujifunza jinsi maadili haya manne yamefika ulimwenguni kupitia kwa Yesu.
More