YouVersion Logo
Search Icon

BibleProject | Tafakari ya Ujio wa YesuSample

 BibleProject | Tafakari ya Ujio wa Yesu

DAY 21 OF 28

Furaha ya Biblia ni uamuzi mkubwa wa imani na tumaini katika nguvu ya maisha na upendo wa Yesu mwenyewe.

Unapoamini kuwa upendo wa Yesu umeshinda kifo chenyewe, kwa kushangaza furaha inakuwa kitu kinachowezekana hata katika hali za dhiki kuu. Hii haimaanishi unapaswa kupuuza au kuficha huzuni. Hilo halifai au wala halihitajiki. Paulo mara nyingi alionyesha huzuni yake kuhusu kuwakumbuka wapendwa au kukumbuka uhuru wake. Aliita hilo kujawa na huzuni na kujawa na furaha bado. Alivyokubali huzuni yake, pia alifanya uamuzi wa Kumwani Yesu. Na kutambua kuwa kupoteza kwake sio mwisho wa simulizi yake.

Soma:

2 WAKORINTHO 6:10

Tafakari:

Unaweza kukumbuka wakati katika maisha yako ulipokuwa umejawa na huzuni lakini bado uliweza kufurahia kabisa? Ikiwa upo, unaweza kuielezea hali hiyo vipi?

Chukua muda sasa ili kumwomba Mungu. Mshukuru kwa furaha yake inayoweza kudumu kuliko huzuni kali zaidi. Mwalike akufundishe jinsi ya kufurahia katikati ya mateso. Mwambie ukweli kuhusu unakopitia ugumu na kumwomba unachohitaji.

Day 20Day 22

About this Plan

 BibleProject | Tafakari ya Ujio wa Yesu

BibleProject ilibuni Tafakari ya Ujio wa Yesu ili kuhamasisha watu mmoja mmoja, vikundi vidogo vidogo, na familia kusherehekea majilio, au kuwasili kwa Yesu. Mwongozo huu wa wiki nne unashirikisha video za kikatuni, mihutasari mifupi, na maswali ya kutafakari ili kuwasaidia washiriki kuchunguza maana ya Biblia ya tumaini, amani, furaha, na upendo. Chagua mwongozo huu ili kujifunza jinsi maadili haya manne yamefika ulimwenguni kupitia kwa Yesu.

More