BibleProject | Tafakari ya Ujio wa YesuSample
Upendo wa Agape kimsingi siyo hisia inayowajia watu. Upendo ni kitendo. Ni uamuzi ambao watu hufanya ili kutafuta ustawi wa wengine. Mtume Paulo katika mojawapo ya barua zake, anasema upendo ni muhimu zaidi ya kuwa na maarifa ya kiroho au uwezo wa kipekee na kwamba hakuna kilicho muhimu bila upendo. Anaendelea na kufafanua jinsi upendo hufikiria na kutenda.
Soma:
1 Wakorintho 13:1-7
Tafakari:
Andika 1 Wakorintho 13:4-7 kwenye kipande cha karatasi. Unavyoandika kifungu hicho kwa mwandiko wako mwenyewe, ni maneno au vifungu vipi vya maneno vinajitokeza kwa upekee kwako?
Unahitaji kuimarika zaidi katika vipengele vipi vya upendo? Mwambie Mungu na uombe msaada wake.
Ukitumia ufafanuzi wa upendo wa Paulo, fikiria kuhusu jinsi ambavyo Yesu amekupenda. Kwa mfano, Yesu amekuwaje na subira, huruma, unyenyekevu na ukarimu kwako?
Ni nani anahitaji ukumbusho kuwa Mungu anampenda leo? Yesu anataka kushiriki upendo wake kupitia kwako vipi wiki hii? Chukua muda ili kuomba kuhusu hilo. Andika mawazo yoyote yanayokuja akilini unapoomba na kufanya mpango wa kushiriki na wengine upendo wake kikamilifu wiki hii.
Scripture
About this Plan
BibleProject ilibuni Tafakari ya Ujio wa Yesu ili kuhamasisha watu mmoja mmoja, vikundi vidogo vidogo, na familia kusherehekea majilio, au kuwasili kwa Yesu. Mwongozo huu wa wiki nne unashirikisha video za kikatuni, mihutasari mifupi, na maswali ya kutafakari ili kuwasaidia washiriki kuchunguza maana ya Biblia ya tumaini, amani, furaha, na upendo. Chagua mwongozo huu ili kujifunza jinsi maadili haya manne yamefika ulimwenguni kupitia kwa Yesu.
More