YouVersion Logo
Search Icon

BibleProject | Tafakari ya Ujio wa YesuSample

 BibleProject | Tafakari ya Ujio wa Yesu

DAY 27 OF 28

Yesu anasema kuwa kiwango cha juu zaidi cha upendo halisi ni jinsi unavyomtendea vyema mtu anayekuvuruga, au kwa maneno yake, “unafaa kumpenda adui wako na kumtendea mema bila kutarajia kupokea chochote.” Kwa Yesu, aina hii ya upendo huiga tabia ya Mungu mwenyewe.

Soma: 

Luka 6:27-36 

Tafakari:

Unatambua nini? Ni maswali gani, mawazo, na hisia zinaibuka unavyosoma?

Kumbuka au simulia simulizi ya uzoefu uliopata wakati wewe au mtu unayemjua, alionyesha upendo kwa adui wake na kutotarajia kupokea chochote. 

Yesu anaahidi nini kwa wanaopenda hivi (tazama mstari wa 35)?

Angalia jinsi Mungu mwenyewe ni mwenye huruma kwa watu wasio na shukrani na waovu. Hili linasema nini kuhusu tabia ya Mungu? Jaribu kufikiria ulimwengu ambapo Mungu ni mkatili kwa watu ambao hawakuwa na shukrani na waovu. Je, yeyote angeokoka?

Angalia jinsi Mungu anavyoelezwa katika mstari wa 36. Kuna uhusiano upi kati ya upendo na rehema? 

Maneno ya Yesu yanakupatia changamoto au kukutia moyo vipi hasa leo? Unaweza kujibu kikamilifu kwa njia ipi leo?

Acha kusoma kwako na tafakuri zichochee sala. Onyesha shukrani zako kwa Mungu kwa upendo wake wa rehema, na kuwa mkweli kuhusu njia ambazo umewanyima wengine upendo huo. Waombee watu ambao wamekutendea vibaya na uombe msaada endelevu wa Mungu ili kupenda kama anavyopenda.

Scripture

Day 26Day 28

About this Plan

 BibleProject | Tafakari ya Ujio wa Yesu

BibleProject ilibuni Tafakari ya Ujio wa Yesu ili kuhamasisha watu mmoja mmoja, vikundi vidogo vidogo, na familia kusherehekea majilio, au kuwasili kwa Yesu. Mwongozo huu wa wiki nne unashirikisha video za kikatuni, mihutasari mifupi, na maswali ya kutafakari ili kuwasaidia washiriki kuchunguza maana ya Biblia ya tumaini, amani, furaha, na upendo. Chagua mwongozo huu ili kujifunza jinsi maadili haya manne yamefika ulimwenguni kupitia kwa Yesu.

More